Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta akizungumza na waandishi 
wa habari juu ya makubaliano na kampuni ya ukandarasi wa ujenzi wa 
kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
MANISPAA ya
 Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imetiliana saini  mkataba  wa 
sh.bilioni 5.56 na kampuni ya ukandarasi  ya  CRJE  ya nchini China  kwa
 ajili ya  kuanza ujenzi wa kiwanda  cha kuchakata taka kuwa mbolea aina
 ya mboji .
Kiwanda hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchakata takaka tani tano (5) hadi 100 kwa siku kitajengwa katika eneo la Mabwepande.
Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini, Dar es Salaam, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta amesema kuwa kiwanda hicho ambacho ujenzi wake unaanza rasmi leo kitakuwa na uwezo wa kuchakata taka ngumu na laini kuwa mbolea aina ya mboji.
Amesema manispaa imekuwa ikitumia kati ya sh.milioni 500 hadi 600 kwa mwezi kugharamia uzoaji wa taka ambazo hizo taka hazizalishi chochote.
Sitta amesema Manispaa ya Kinondoni inazalisha tani 22,000 kwa siku hivyo kutumia fedha nyingi kuwalipa makandarasi.
Amesema zaidi ya wananchi 1000 wanatarajiwa kunufaika na ajira kupitia kiwanda hicho.
Aidha amesema hatua hiyo kubwa ya kuitikia sera ya taifa ya kuelekea uchumi wa viwanda na kinondoni tunakuwa kuzalisha mbolea aina ya mboji ambayo haina madhara katika udongo ukilinganisha na mbolea za kemikali,”.
Meneja wa Kanda wa kampuni ya CRJE, Bai Haochen amesema, ujenzi wa kiwanda hicho unaweza kuchukua muda wa miezi 12 hadi 18.

 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa 
kampuni ya CRJE,  Bai Haochen wakitiliana saini ya makubaliano ya ujenzi
 wa kiwanda cha kuchakata taka na kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
Meya
 wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa kampuni
 ya CRJE,  Bai Haochen wakibadilishana hati za makubaliono leo jijini 
Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment