HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 12 October 2017

TAASISI YA' ROOM TO READ ' YAMPA TUNZO MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

MKE wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete  jana alikabidhiwa  tuzo ya heshima kutokana na kutambua jitihada zake za kumlinda na kumtetea mtoto wa kike  iliyotolewa na  Taasisi isiyo ya Kiserikali inayifahamika kwa jina la Room to Read.

Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo  Mkurugenzi wa Room To Read  Peter Mwakabwale kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Bwawani Kihaba Maili Moja Mkoani Pwani.

Akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka katika shule mbalimbali za mkoa  wa Pwani mama  Kikwete amezitaka Hamlashari kutenga bajeti ya kujenga mabweni katika shule kwa ajili  ya wanafunzi wakike  sanjari  na kujenga  maabara  na vyumba  vya madarasa  ili kuweza  kuwarahisishia  wanafunzi  hususani wasichana  ili waweze kujifunza  bila  kikwazo chochote na kufaulu vema masomo yao.
Aidha  Mama Salma Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi  katika   maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike  duniani ambayo yameadhimishwa  kimkoa Kibaha Mkoani Pwani.
Mama Salma Kikwete amesema kuwa  Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya kumi  kitaifa kwa mimba  huku sababu mojawapo ni  ukosefu wa mabweni ya wasichana hali inayopelekea wasome shule za kutwa na kukutana na vishawishi wawapo njiani kuelekea ama kurudi shule.
Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room to Read linaloendesha mradi wa Elimu kwa Wasichana  katika mkoa wa Pwani  na  kuzihusisha  Wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Kibaha ambapo wamekuwa wakitoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana lakini pia kuwasaidia gharama za mahitaji ya shule pamoja na karo kwa familia zisizo na uwezo wa kifedha 
 Siku ya kumuenzi mtoto wa kike  huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 11 kufuatia  maazimio  ya malengo endelevu  ya Umoja wa mataifa , viongozi  wa nchi mbalimbali  duniani  walikubaliana  na kuyapitisha   huku miongoni mwa malengo  matano   mojawapo  kuhakikisha  tunafikia usawa  wa kijinsia  na uwezeshaji  wa wasichana  na wanawake  wote  duniani ifikapo mwaka 2030.

Wahamasishaji wa Mradi wa Elimu kwa wasichana Room to Read wakionesha kazi wanazozifanya katika maadhimisho ya mtoto wa Kike duniani October 11 mkoani Pwani -kibaha

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad