HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 17, 2017

TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA YAMWONYA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI

  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Valentino Mlowola akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati alipokuwa akiwaonya wabunge watatu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema).

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wamemuonya mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari kuacha kuwashinikiza kufanyia kazi ushahidi wa rushwa aliopeleka katika chombo hicho bali awaache wafanye kazi.

Aidha wamesisitiza kuwa, ushahidi aliopeleka Mbunge Nasari akiongozana na Lema pamoja na Msigwa siyo ushahidi bali ni taarifa ambayo bado wanaifanyia kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Valentino Mlowola amesema suala alilolipeleka Nassari katika Taasisi hiyo siyo suala la kisiasa bali ni la kisheria lakini anachokiona Nasari na wenzie wanataka kulifanya suala hilo kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria.

“Namuonya Mh. Nassari ameishaleta taarifa zake kwetu atuachie tufanye yale tunayopaswa kufanywa kwa mujibu wa sheria na siyo kutushinikiza, kama kauli waliyotoa jana, nitaendelea kuwa natoa series kutokana na  sisi tunavyofanyakazi, hii ni Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote tukiangalia sheria tuko huru kufanya majukumu yetu na hapashwi hata mara moja kutushinikiza”. Amesema Mlowola.

Ameongeza “endapo ataendelea na utaratibu huu sheria itachukua mkondo wake bila kuathiri taarifa zake alizozileta”.

Amesema, katika ushahidi kuna mambo mengi,  wanaangalia matakwa ya kisheria, kwani ushahidi una sifa, kuna swala la relevance na vissibility kwa hiyo na kusisitiza kuwa walichopokea kwa Nasari ni taarifa inayotakiwa kufanyiwa kazi na siyo ushahidi.

Ameongeza kuwa, taasisi hiyo, inapokea taarifa zinazohusiana na rushwa au  makosa ya rushwa kutoka vyanzo mbalimbali vikiwemo vya wazi na vya siri na sheria inataka mtoa taarifa alindwe lakini Nasari yeye aliamua kufanya vikao na waandishi wa habari kwa mara zote tatu alizofika Takukuru na hata kufikia kutoa taarifa juu ya hatua zinazoendelea katika mchakato huo.

Aidha, Mlowola amemshangaa Nassari kuuliza kwa nini hawajaupeleka ushahidi huo mahakamani mpaka sasa na kusema wao wanaongozwa na sheria ya mwenendo wa mashtaka na wakishamaliza uchunguzi watatathimini matokeo waliyoyapata na wakijiridhisha walichopewa kinakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria watafikisha katika hatua stahiki ya kupeleka jalada kwa DPP ambaye akiridhika na ushahidi ataandaa mashtaka dhidi ya washtakiwa na kupelekwa mahakamani.

“Kuna matukio yanafanyika na watu wanadhani ni makosa kumbe ni 'moral wrongs' tu amabayo yanahitaji utaratibu mwingine wa kuwashughulikia”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad