HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 12 October 2017

RC Rukwa aitahadharisha TARURA kutorudia makosa ya Halmashauri. Inbox x

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameitahadharisha Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa yanafanywa na Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.

Amesema kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo kujengwa chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya matengenezo ya mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali imeamua kuzitafutia ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.

“Ukiitwa Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka hata sisi ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya kiwango, na hapo mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana kwenye barabara lakini kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua zinataka kuanza ndio utaona mkandarasi anaingia barabarani kwenda kutengeneza barabara,” Mh. Zelote alifafanua.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Amesisitiza kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua za kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

Hivyo ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu na kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara, (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule pamoja na Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad