HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 27, 2017

RC MAKONDA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA SHOWROOM ZA MAGARI KIGAMBONI

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni ,Hashim Mgandilwa,vinongonzi mbalimbali  wakiangalia ramani ya eneo maalumu lililotengwa Kigamboni kwajili ya Showroom zote za Magari jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana ametembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa miundombinu  kwaajili ya Showroom zote za Magari kwenye eneo Maalumu lililotengwa Kigamboni.

RC Makonda ameongozana na viongozi wa Taasisi mbalimbali ikiwemo TRA, SUMATRA, NSSF, Bank ya watu wa Zanzibar pamoja na Jeshi la Polis na Jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao wameenda kuonyeshwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi.

Makonda amesema kuwa lengo kuhamishia Showroom Kigamboni ni kufanya Kigamboni kuwa soko la Magari Africa, kuwapa Wananchi fursa ya kuchagua gari analotaka kwenye  eneo moja, kuiwezesha Serikali kupata mapato na kupunguza wizi wa magari.

Akiwa kwenye eneo hilo ameshuhudia ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Madaraja, Umeme na Maji ikienda kwa kasi kubwa.

Tayari baadhi ya Taasisi na wenye Showroom waliokabidhiwa maeneo wameanza kujenga ili kuhakikisha ifikapo January Mosi wanakuwa wamehamisha Showroom zao.



Ndani ya eneo hilo kutakuwa na ofisi za Taasisi zote zinazohusiana na biashara ya Magari ikiwemo TRA, TPA, SUMATRA, Bank, NSSF,Bima, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na uokoaji, Garage, Sheli na Wauzaji wa Vipuri vya Magari.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni ,Hashim Mgandilwa,viongonzi mbalimbali  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu  katika eneo maalumu lililotengwa  kwaajili ya Showroom zote za Magari.(Picha na Emmanuel Massaka,Glob ya jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad