HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 7 October 2017

Promosheni ya Shinda Tiketi na ‘Zali la Mwanaspoti’ yaziduliwa jijini Dar

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications,Francis Nanai(kutoka kushoto),Mhariri mtendaji wa magazeti ya Mwananchi Communications, Bakari Machumu, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka Kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba, Meneja Masoko Azam tv, John Mbele na Meneja Masoko Mwananchi Communications, Sarah Munema wakiwa na baadhi ya zawadi zitakazotolewa katika promosheni ya kuwazawadiwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti katika kipindi maalumu cha Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya SportPesa, Tarimba Abbas akizungumza katika hafla ya promosheni ya kuwazawadiwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti katika kipindi maalumu cha Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu akizungumza akizungumza katika hafla ya promosheni ya kuwazawadiwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti katika kipindi maalumu cha Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wageni na wafanyakazi wa MCL wakiwa kwenye Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.

Gazeti maarufu la michezo nchini, Mwanaspoti, linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL),  limezindua promosheni maalumu inayofahamika kama Shinda Tiketi na ‘Zali la Mwanaspoti’.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mhariri Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu, alisema kuwa, promosheni hiyo inalenga kuwazawadia wasomaji wake, ambao wengi wao ni wapenzi wa michezo na burudani kujishindia zawadi mbalimbali, lakini pia kupata habari bora zaidi za michezo na burudani.

Promosheni hii inakuja wakati ambapo, Gazeti la Mwanaspoti ambalo pia huuzwa nchini Kenya, likiwa limefanyiwa maboresho ya kina ikiwamo kubadili mwonekano, kuongeza safu za wachambuzi mahiri, wanamitindo maarufu na wasifu wa wanamichezo maarufu  kutoka nje na ndani ya Tanzania. 

Kwa mujibu wa Machumu, lengo la MCL ni kuhakikisha kuwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti wanapata habari zilizo bora na zinazokwenda na wakati na pia zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wa kina.

Alisema Machumu, katika promosheni hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na zawadi za kila siku, wiki na  za mwisho wa promosheni.

Zawadi za kila siku ni pamoja na fulana na mipira ya miguu, jezi za timu mbalimbali za ligi kuu ya Uingereza. Wakati  zawadi wiki ni ving’amuzi vya Azam TV ambavyo vimeunganishwa na vifurushi vya bure kwa muda wa mwezi mmoja pamoja na pikipiki, simu za mkononi pamoja na bodaboda pamoja na washindi 8 watakaopatikana katika droo ya kila wiki, ambao watapata fursa ya kwenda Uingereza kushuhudia mechi mojawapo dhidi ya timu kubwa katika ligi kuu nchini humo.

Kati ya washindi hao nane , mshindi wa droo kubwa ya mwisho wa promosheni  atapata nafasi ya kuchagua rafiki yake atakayetaka kusafiri naye kushuhudia mechi hizo kabambe.

Droo za kila wiki zitakuwa zinarushwa kupitia televisheni ya Azam kwenye kipindi cha michezo cha Mshike Mshike kila Jumatano.

Promosheni hii inadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa, ambapo Mkurugenzi wake, Abbas Tarimba, alisema kuwa lengo la kudhamini safari hiyo ni kuongeza hamasa ya watanzania kupenda michezo.

Mdhamini wa pili ni Azam ambapo, Mwakilishi wake, John Mbelle ambaye ni Meneja Mauzo, alisema kuwa wameamua kudhamini promosheni hiyo kama wadau wa michezo nchini na pia kutoa ving’amuzi ili watanzania wapate fursa ya kushuhudia michezo mbalimbali kupitia Azam TV.

Machumu aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kusisitiza kuwa, droo ya kwanza itafanyika baada ya wiki mbuili. “Hii ni fursa pekee na sisi tutafanya droo zetu kuanzia Mwezi Oktoba chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha,” alisema

Machumu alimaliza kwa kutaja gharama za kampeni nzima hii ya “Zali la Mwanaspoti kuwa itagharimu shilingi milioni mia tatu (300,000 000/=).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad