HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 30, 2017

NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA WAFUGAJI WA OLOLOSOKWAN KUWA NA UTULIVU KUSUBIRI UTATUZI WA MGOGORO WAO NA HIFADHI

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha juu ya kuwa watulivu wakati suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wafugaji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kuwa watulivu wakati suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Naibu Waziri Ulega ameeleza hayo jana katika mkutano na wafugaji hao uliofanyika kwenye Kata ya Ololosokwan wilayani humo.

“Wakati tunamsubiri Waziri Mkuu atoe maelekezo naomba msiharibu hali ya hewa hii ndiyo rai yetu.Au kuna yeyote anayepinga jambo hili? Aliwauliza wafugaji hao na kujibiwa hakuna na wote wapo pamoja na Serikali.

“Hatua hii itaturahishishia sisi kwa sababu wizara inaliangalia jambo hili kwa ukaribu kutokana sehemu kubwa ya nchi wafugaji wamekuwa malalamiko makubwa sana ikiwamo kufilisia mifugo yao pindi inapoingia hifadhini na kusababishiwa umasikini,”amesema Ulega.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alimweleza Ulega kwamba ukosefu wa malisho ni mojawapo ya changamoto inayowakabili wafugaji hao kutokana maeneo machache yaliyopo.

Hata hivyo, Ulega alihaidi kulishughulikia changamoto hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja watatafuta mashirika kwa ajili kuangalia namna ya kuboresha malisho hayo ili kuleta ahueni kwa wafugaji hayo.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisalimina na wazee wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mmoja wa wafungaji Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka akizungumza na wananchi wa kata ya Ololosokwan mkoani Arusha.
Wanana wa kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii,Arusha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad