HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 2 October 2017

NAIBU WAZIRI MABULA ASEMA JUKUMU LA KUPANGA MIJI KWENYE HALMASHAURI HALIEPUKIKI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuweka utaratibu wa kupanga miji kama sehemu ya kazi yao kuliko kukurupuka na mashinikizo ya makundi ya watu.

Naibu Waziri Mabula amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa madhimisho ya siku ya Makazi Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee.

“Halmashauri ndio zinajukumu kubwa la kupanga miji lakini cha ajabu Halmashauri nyingi zimekuwa zikipima miji kwa mashinikizo ya makundi hali inayofanya kuibuka kwa miji holela mingi katika makazi yetu” Amesema Mabula.Waziri Mabula ameongeza kuwa siku ya makazi inatukumbusha umuhimu wa kuwa na makazi bora yanayoendana na miundombinu ya huduma za kijamii.

Ameweka wazi kuwa kwa sasa Wizara yake imeweza kurasimisha nyumba zaidi ya 2000 katika eneo la Kimara na Mbezi lakini haijamaanisha kuwa zoezi hilo litaweza kuendelea nchi nzima katika maeneo ambayo yamejengwa kiholela.

Ametaja kuwa serikali itaendelea kusimamia mpango kabambe(Master Plan) wa miji yote hivyo hawatakuwa na msamaha kwa wote watakaokwenda kinyume na utaratibu wa mpango huo .

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , John Lupala akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Angelina Mabula akizungumza na wadau wakati wa maadhimisho ya siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Ushirika wa Nyumba (Mwenge) wakijadili jambo katika Mahadhimisho ya siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam.
Wajumbe wa Ushirika wa Viguta wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri , Angelina Mabula

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad