HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 14 October 2017

NAIBU WAZIRI INJINIA STELLA MANYANYA ZIARA MKOANI DODOMA

Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya amefanya ziara yake ya kwanza ya kikazi akiwa kwenye Wizara ya Viwanda kwa kutembelea kiwanda cha ngozi na bidhaa za ngozi katika eneo la Zuzu Mkoani Dodoma.
Aidha Mhe. Waziri amewaagiza watendaji wa wizara kufanya juhudi za haraka za uendelezwaji wa eneo hilo kwa kuwa hakuna sababu ya kuchelewa ambapo Naibu waziri ametoa muda wa miaka miwili eneo hilo liwe limeanza kuwekewa miundombinu na huduma nyingine.
Pia   Injinia Stella Manyanya alitembelea eneo la SIDO lililotengwa kwa ajili ya kiwanda cha alizeti ambapo pia amewaagiza watendaji kufanya juhudi za haraka kuharakisha mchakato wa uendelezwaji wa eneo hilo, Mhe. Naibu waziri alihitimisha ziara yake kwa kutembelea ofisi za SIDO na kutembelea ajasiliamali walioko chini ya SIDO na kujionea shughuli za ujasiriamali zinazofanywa katika eneo hilo.
Mhe. Naibu waziri ataendelea na ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara kuanzia wiki ijayo na kujionea utendaji wa kila taasisi.
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akizungumza na watendaji wa SIDO, Dodoma alipowatembea na kukaguashughuri zinazofanywa wajasiriamali wa mkoani humo.
 Darasa maalumu la mafunzo ya uzalishaji na utengezaji wa bidhaa za ngozi lililopo Kizota, mkoani Dodoma.
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akishuhudia bidhaa mbalimbali zinazotengezwa na wanafunzi wanaojifunza utengezaji wa bidhaa za ngozi, Kushoto ni Meneja wa mafunzo SIDO mkoani Dodoma, Stephano Ndunguru.
 Baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengezwa na wanafunzi wanaojifunza utengezaji wa bidhaa za ngozi katika kiwanda cha SIDO mkoani Dodoma
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akiangalia bidhaa zinazotengezwa na wajasiriamali wa SIDO.
 Baadhi ya bidhaa za zilizotengenezwa na wajasiriamali wa SIDO, mkoani Dodoma
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akichomelea alipowatembelea wajasiriamali wa vyuma SIDO, Dodoma.
 Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akizungumza na waamdishi wa habari alipotembelea SIDO, Dodoma kujionea shughuri mbalimbali zinazofanywa na SIDO.
Naibu waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stellah Manyanya akikagua eneo maalumu kwa ajili ya kongano la ngozi, Zuzu mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad