HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 21 October 2017

MSANII WASTARA AZINDUA FILAMU YAKE MPYA YA KIBWEBWE

Mkurugenzi wa kampuni ya J Films Wastara Juma akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa filamu ya KIbwebwe iliyo chini ya kampuni yake sambamba na kumtambulisha msanii wake mpya wa miondoko ya singeli Charles Fidelis 'Chaz K' (kushoto) 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MKURUGENZI wa kampuni ya uandaaji filamu ya J Films na muigizaji wa maigizo ya sanaa nchini Bongo Movie Wastara Juma amesema malengo yake ni kuuza filamu zake nje ya nchi na hio linawezekana kama watakuwa wanatengeneza filamu zenye ubora mzuri.

Akizungumza na waandishi wakati wa ufunguzi wa filamu ya KIBWEBWE inayosimamiwa na kampuni yake, Wastara amesema kuwa katika kampuni yao kuna kazi tatu zilizokuwa tayari ila kwa pamoja wakaona ni vizuri wakianza na filamu ya Kibwebwe na itaenda zaidi kimataifa.

Wastara amesema kuwa, filamu hiyo ni ya maisha halisi ya mwanamke wa ktanzania na kiafrika na inaweza kuangaliwa na mtu yoyote mwenye rika lolote pia ina mafunzo yatakayompa mtu elimu ya kimaisha.

"Ni mara yangu ya kwanza kuzindua filamu hii na matarajio yangu ni kwenda kimataifa zaidi, pia nimefurahia kuifanyia nje ya Tanzania nina imani kila mtu ataipenda kwani ni filamu nzuri, sio ndefu na haichoshi sana katika kuangalia na ikizingatia maadili kila rika lina uwezo wa kuiangalia filamu hiyo na kufurahi,"amesema Wastara.

Wastara amesema kuwa filamu hiyo pia itapelekwa katika nchi za Uingereza na Canada na itaanza kuuzwa rasmi nchini baada ya mwezi mmoja.

Mbali na uzinduzi wa filamu ya Kibwebwe, Wastara amemtambulisha msanii wake mpya anayeimba nyimbo kwenye miondoko ya Singeli na wameingia makubaliano ya kumsimamia nyimbo zake, Msanii huyo Charles Fidelis 'Chaz K' ametambulisha nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la Mtaani Kwetu akisema kuwa huo ni mwanzo kwani bado ana nyimbo nyingi na zenye ubora mzuri.

"Nimeamua kuachia nyimbo yangu hii kwa sasa nikiwa chini ya meneja wangu mpya Wastara ambaye atakuwa anasimamia kazi zangu zote, pia bado nina kazi zingine ni nzuri na zitakuja kuingia kwenye soko la ushindani hususani kwenye mziki wa miondoko ya singeli," amesema Chaz K.
Msanii wa miondoko ya singeli Charles Fidelis "Chaz K" akimshukuru Meneja wake Wastara Juma kwa kuamua kumsimamia kazi zake kwa sasa na tayari akiwa ameshatengeneza kazi mbalimbali na kuitambulisha nyimbo yake mpya inayojulikana kama mtaani kwetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad