HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 9, 2017

MSANII ALIKIBA WA TANZANIA NA PATORANKING WA NIGERIA WAFANYA KWELI COKE STUDIO


 Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wanaendelea kupata burudani ya muziki kutoka wasanii nguli kutoka nchi za afrika kupitia onyesho la Coke Studio kupitia luninga ya clouds ambapo mwishoni mwa wiki Kolabo ya mwanamuziki nguli kutoka nchini Ali Kiba na mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Patoraking, imeacha gumzo kubwa.

 Kolabo hiyo ambayo imesukwa na msanii nguli wa kutengeneza muziki wa studio kutoka Nigeria,MasterCraft, ina mvuto mkubwa kwa watazamaji hususani vipao vya wanamuziki hawa vya ‘Chekecha Cheketua’ na ‘My Woman My everything’ ambavyo wameviimba kwa kushirikiana sambamba na kucheza pamoja kwenye jukwaa.
Wanamuziki wengine waliopagawisha washabiki wa muziki katika onyesho hilo la tano ambao muziki wao umetengenezwa studio na msanii wa muziki wa studio kutoka Afrika ya Kusini ni SupaMega kutoka nchini Afrika ya Kusini,Olamide King Baddo kutoka nchini Nigeria na bendi ya Beca inayoundwa na wasanii wawili machachari wa muziki,Becky Sangolo na Carol Kamweru kutoka nchini Kenya.

Wakitoa maoni yao kuhusiana na onyesho hili,baadhi ya wapenzi wa muziki kutoka mikoa mbalimbali wanaolifuatilia walisema kuwa burudani za Coke Studio msimu huu ni moto wa kuotea mbali kwa kuwa kolabo za wanamuziki zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba zikionyeshwa zinaleta furaha na kumfanya mtazamaji kujiona anaangalia onyesho la wanamuziki hao mubashara (Live) Mbali na wasanii wa Tanzania,wasanii msimu huu wa tano wa Coke Studio unawajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon.
Baadhi ya wasanii hao ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda ( Uganda).Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana.

 Tangia onyesho hili lianze kuonyeshwa mwezi uliopita limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad