HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 17 October 2017

MAZINGIRA BORA YAWEKWA NA SERIKALI KWA WAWEKEZAJI

 Mkuu wa kitengo cha Mawsiliano kampuni ya simu za mkononi ya Halotel, Mhina Semwenda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Kusoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh.
  Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala.
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni
Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh

 KAMPUNI ya Simu ya Mkononi ya Halotel imesema kuwa serikali imeweka mazingira bora kwa wawekezaji kupitia vyombo vyake ambavyo vimefanya Halotel kupata mafanikio katika kutoa huduma ya mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh amesema Halotel imetimiza miaka miwili tangu ilivyoanzishwa mwaka jana Oktoba 15.
Amesema kuwa katika mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka miwili ni kuwa na wateja zaidi ya milioni 3.5  wanaotumia mtandao  huo katika mawasilino.

Than Binh, amesema kuwa katika miaka miwili ya utoaji huduma, wamefanya mapinduzi na mabadiliko makubwa katika sekta hiyo katika nyanja za Mawasiliano ikiwemo kuboresha miundombinu ya Mawasiliano, Mabadiliko katika Elimu, huduma za kifedha pamoja na kupunguza gharama za mawasiliano.

“Tangu tumeanza kutoa huduma kwa mwaka wa pili sasa idadi ya wateja imeendelea kuongezeka kwa kasi. Hii inatokana na huduma ambazo tumekuwa tukizibuni kwa pamoja na kuwekeza zaidi katika kutoa huduma bora na kuboresha miundombinu ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini.” Amesema

“Kwanza tunafurahishwa na Serikali kutokana na mazingira bora ya uwekezaji ambayo imeweka hadi sasa,  na pia mazingira mazuri ya ukusanyaji wa kodi kwa uwazi zaidi suala ambalo hata kwetu limeondoa usumbufu kwa kiasi kikubwa, kuzinduliwa kwa kituo cha ukusanyaji kodi kwa njia ya kielectroniki ilikuwa faraja kubwa kwetu na ndio maana tulikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza za simu kujiunga na mfumo huo.”

Binh, amesema kuwa wamefurahi pia kuwa kampuni inayoongoza kwa kutoa ajira kwa Maelfu ya Watanzania ikiwa ni ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu moja na mia mbili 1200, na ajira zisizo za moja kwa moija zaidi ya Elfu Ishirini 20000 na kusema kuwa kutokana na uwekezaji ambao kampuni hiyo imeendelea kufanya wanaamini wataendelea kuongeza idadi ya ajira nchini.

Aidha Binh, aliongeza kuwa wanaamini bado wana nafasi kubwa zaidi ya kufanya uwekezaji na kubadili kabisa mfumo wa Mawasiliano nchini kwa kuanzisha njia mpya za mawasiliano kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi na kuwa kampuni itakayo ongoza katika utoaji wa huduma za Mawasiliano kupitia Tehama na Teknolojia ya Mawasiliano.

Amesema wanaelekea kuanzisha mtandao wa 4G LTE kwa wateja wetu wote wa Halotel, hatuta bagua maeneo tutafanya uwekezaji huu katika maeneo yote nchi nzima ili wateja wetu waweze kufurahia huduma bora za mawasiliano na kwa bei rahisi,” alisema na kuongeza, “Pia tunaangazia sekta ya elimu ambayo hadi sasa kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar Es Salaam, tumeweza kuanzisha mfumo wa kujisomea kwa shule za sekondari nchini kwa masomo ya Sayansi Mfumo ambao utapatikana bure kwa shule zote zinazotumia Mtandao wa Intaneti wa Halotel, Tumeanza na masomo ya sayansi na kadri muda unavyokwenda tutaangalia namna ya kuingiza masomo mengine, baada ya kukamilisha kutia saini Mkataba wa Maelewano kati yetu na Wizara ya Utawala bora TAMISEMI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad