HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 11 October 2017

MAMBO SITA MUHIMU UNAPOPEKULIWA NA ASKARI.

Na Bashir Yakub.
Unapopekuliwa yapo mambo ambayo usipoyazingatia wewe unayepekuliwa basi yatakuingiza matatani mbeleni au hata kama umebambikiziwa kosa itaonekana ni kweli na waweza kwenda jela bila kuwa umetenda kosa lolote.
Kawaida wanaopekua ni askari. Usitarajie huyu anayekuja kukupekua awe ndiye wa kukwambia haki zako . Badala yake wewe unayepekuliwa ndiye uwe wa kumwambia askari kuwa hiki ndicho hiki hapana. Askari anapokuja kukupekua tayari wewe unashukiwa na hivyo ni rahisi kwake kuacha kufuata au kuongeza jambo lisilokubalika ilimradi atimize lengo lililomleta. Wewe ndiye wa kusema hili ndio na hili hapana. 


Hivyo basi ni muhimu sana kwako kujua kuhusu kupekua na mambo gani ya msingi ufanyiwe au usifanyiwe ili kuepuka uwezekano wa kwenda jela bila kosa.

Usiseme mimi sina haja ya kujua kuhusu kupekua kwasababu ni mwema sana na hivyo si rahisi kutakiwa kupekuliwa. Laa hasha, kupekuliwa na kukamatwa na polisi humkumba yeyote awe mwema ama vinginevyo. Kujua ni silaha na hivyo ni muhimu kukaa na silaha hii.  

Makala yatapitia sura ya 20, vifungu vya 38 hadi 45 vya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai .


1. NANI ANARUHUSIWA KUKUPEKUA.

Askari ndiye anayeruhusiwa kukupekua. Hata raia wanaweza kumzuia raia mwenzao wakampekua ikiwa wana taarifa kuhusu kuficha au kumiliki kitu ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria. Isipokuwa ni haramu kabisa kwa raia kumpekua raia mwenzake bila kuwa na kibali maalum.

2. VITU GANI VINAWEZA KUPEKULIWA.
Mtu kama mtu anaweza kupekuliwa, kwa maana nguoni mwake kama mifukoni nk. Pia vifaa kama gari, ,meli, nk navyo vyaweza kupekuliwa. Halikadhalika nyumba kama nyumba nayo yaweza kupekuliwa pamoja navyo vifaa vingine.


                 KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad