HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 10 October 2017

MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salam leo Oktoba 10 2017 alipotoa takwimu za makusanyo ya zaidi ya Trilioni 1 kwa Mwezi kwa mamlaka hiyo kwa miezi ya Julai, Agosti na Septemba 2017. Pamoja naye Maafisa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa taarifa ya makusanyo ya mapato ya kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2017, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.65.

Makusanyo haya ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Katika kipindi hicho cha miezi mitatu, makusanyo ya kila mwezi yalikuwa kama ifuatavyo;-

Julai, 2017 Shilingi 1,101,193,417,551.91

Agosti, 2017 Shilingi 1,205,008,256,053.51

Septemba, 2017 Shilingi 1,345, 339,916,757.65
Kwa makusanyo haya, Mamlaka ya Mapato Tanzania, inapenda kuwashukuru wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kwa kuendelea kulipa kodi na kuiwezesha serikali kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, Mamlaka inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki kwa kila mauzo na kudai risiti kwa kila manunuzi kwani ni njia pekee ya kupata mauzo sahihi yanayoiwezesha TRA kukokotoa kodi sahihi na kwa haki.

“Napenda kuwakumbusha wananchi wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wa tarehe na kiasi walicholipa na bidhaa waliyonunua kabla ya kuondoka na risiti hiyo. Endapo utaona haina vigezo tafadhali ripoti kwenye ofisi ya TRA iliyokaribu nawe au piga simu kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba 0800750075 au 0800780078. anasisitiza Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

Vile vile, Mamlaka inawakumbusha wamiliki wa majengo nchini kulipa kodi ya majengo mapema badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka wa fedha ili kuepuka misongamano na usumbufu usio wa lazima.

Pia, wafanyabiashara wa michezo ya kubahatisha wanapewa wito wa kulipakodi zao kwa mujibu wa sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41.
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu.Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salam leo Oktoba 10 2017 alipotoa takwimu za makusanyo ya zaidi ya Trilioni 1 kwa Mwezi kwa mamlaka hiyo kwa miezi ya Julai, Agosti na Septemba 2017. Pamoja naye afisa kodi Mkuu, Julius Ceaser.
kodi wakuu, Julius Ceaser (kushoto) na Sydney Mkamba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad