HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 13 October 2017

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA DR.MOKIWA KUPINGA KUVULIWA UASKOFU NA KUONDOLEWA KWENYE ORODHA YA WADHAMINI WA KANISA.

Mahakama Kuu, Dar es Salaam leo tarehe 13 Oktoba, 2017 imetupilia mbali kesi Na. 52 ya mwaka 2017 iliyofunguliwa  Mahakamani hapo na aliyekuwa Askofu wa Dar es Salaam, Dkt Valentino Leonard Mokiwa ikiwa ni sehemu ya hatua za kupinga kuvuliwa  uaskofu iliyofikiwa  tarehe 7 Januari, 2017 na Askofu Mkuu wa Kanisa la Angalikana Tanzania kutokana na tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya uaskofu na Katiba ya Kanisa hilo. 

Kesi hiyo iliwasilishwa Mahakama Kuu Tanzania  dhidi ya Kabidhi Wasii Mkuu (RITA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wadhamini wa Kanisa la Angalikana Tanzania kupinga maamuzi ya RITA kumwondoa kwenye orodha ya wadhamini baada ya kuvuliwa uaskofu.

Mahakama Kuu imeona kuwa,  kesi  ya Dr. Mokiwa  imefunguliwa kinyume cha Sheria kutokana na sababu moja kati ya nyinginezo kwamba maombi yaliletwa mahakamani kwa kutumia vifungu vya sheria visivyo sahihi (wrong citation of the law).

Mahakama imemuaru pia Dr. Mokiwa kulipa gharama za kesi hiyo. 

Kabla ya shauri hilo Mahakama Kuu, Dr. Mokiwa aliwahi tena kufungua kesi katika Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutetea nafasi ya uaskofu na kesi hiyo iliondolewa kwa kukosa uhalali Mahakamani.

Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo wameeleza kuwa aina ya kesi iliyofunguliwa inahusu masuala ya kiroho na hivyo, haikustaili kwa mlalamikaji kuyaleta Mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad