HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 14 October 2017

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA NYERERE YAFANA TEMEKE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva (wa katikati) akiwa sambamba na watumishi wa serikali wa manispaa hiyo na vikundi vya mazoezi ya Jogging katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Hayati Mwalim Julius Nyerere leo uwanja wa Taifa  Jijini  Dar es salaam.

Katika kuadhimisha siku ya kumbumbuku ya hayati Baba wa Taifa Mwl; Julius Kambarage Nyerere, Wilaya ya Temeke yafanya michezo mbalimbali ambayo ilijumuisha watumishi wote wa Wilaya hiyo na vilabu vyote vya michezo vya Mkoa wa Dar.

Mgeni rasmi wa tamasha hilo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva alifurahishwa na kazi nzuri ya maandalizi ya Tamasha hilo, jinsi watumishi na vilabu vya michezo walivyojitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hiyo ya kifo cha baba wa taifa.

Lyaniva alisisitiza kuyaishi maisha ya Mwl Nyerere  kwa kuwa wazalendo wa taifa letu na kuikataa rushwa ambayo ni adui wa maendeleo na adui wa haki. 

Alisema "Mwalimu Nyerere alikua mpenzi wa michezo ndio maana leo tunamuenzi". Mwl Nyerere ndiye alikua muanzilishi wa michezo mbalimbali. 

Alisisitiza katika vilabu vyote vya michezo kuwa na shughuli mbalimbali za kijasiliamali ili kujikwamua kiuchumi.

Alisema hayo alipowakumbusha wanamichezo kuwa pamoja na kwamba michezo ni afya lakini pia ikitumiwa vizuri itakuinua kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva na watumishi wa serikali wa manispaa hiyo pamoja na vikundi vya mazoezi wakifanya mazoezi ya pamoja.
Wakishiriki michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia ndani ya magunia.
Watumishi wa manispaa ya Temeke wakifurahi kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad