HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 23 October 2017

KAMPUNI YA KILUA INDUSTRIAL GROUP YAANDAA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING,NCHINI CHINA

Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies imeandaa kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa  kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Mohamed Said Kilua amesema kuwa kongamano hilo linatarajia kufanyika Oktoba 25,2017 katika hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano jijini Beijing,litakalojumuisha wafanyashabiashara wamiliki wa viwanda na makampuni  wapatao 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.

“Sisi Kilua Industrial Group of Companies tumeamua  kuibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda, na kwa njia moja ama nyingine iweze kuzigeuza rasimali maliasili  kuwa bidhaa”alisema Kilua.

Tanzania iliyojaaliwa ardhi yenye rutuba kwa kilimo cha mazao ya Chakula na Biashara,haiwezi kutafsiri maendeleo hayo ya Kilimo bila kuzigeuza bidhaa zilizoandaliwa kwa soko la ndani na lile la Kimataifa bila kuwepo na viwanda vidogo/vya kati na vikubwa vitakavyozalisha bidhaa zenye viwango vyenye ubora katika ushindani wa soko”alisisitiza Kilua.
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua (pichani shoto) pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali ya mkoa wa Pwani wakipatiwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huateng Metalluargical Co.Ltd, Chunsheng Jiang (wa nne kulia) kuhusiana na michoro waliyopewa kama zawadi, ikionesha mandhari ya maeneo mbalimbali ya jiji la Beijing pamoja na shughuli zao nchini China.

Viongozi hao ni Mkurugenzi wa halmashauri Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani (kofia nyekundu), Mansouly Ally ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha, Afisa Biashara (M) Pwani Suleiman Sirindwa, Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Mhina. 

Viongozi hao wamekuja jijini Beijing nchini China kwa ziara iliyoratibiwa na Kampuni ya Kiluwa Group of Companies,chini ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wake Mohamed Said Kiluwa (mwenye koti la njano) kwa ajilia kushiriki Kongamano kubwa la Viwanda. 
Aidha baada ya kukutana leo viongozi hao pamoja na wadau wakuu wa mambo ya viwanda nchini China, ambapo Oktoba 25 kutakuwepo na Kongamano litakalohusu masuala ya viwanda,litakajumuisha wadau wapatao 200 kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhina akikata kipande cha nyama ya Mbuzi,ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha wageni na wenyeji kwenye chakula cha jioni kiliochoandaliwa na wenyeji wa Beijing,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua,kulia ni Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja na Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga wakishuhudia tukio hilo usiku huu.
 Baadhi ya wenyeji ambao nao wanatarajiwa kushiriki kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika Octoba 25,2017 chini ya Uratibu mkubwa wa kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies,jijini Beijing nchini China.
 Wageni wakipewa maelezo mafupi katika baadhi ya michoro ambayo walipewa kama zawadi kutoka kwa wenyeji wao,kabla ya kupata chakula cha jioni pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad