HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 22 October 2017

JTFE YAKABIDHI MSAADA ULIOTOLEWA NA WATU WA ISRAEL KWA WATOTO WENYE UALBINO KITUO CHA BUHANGIJA - SHINYANGA


Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) inayojihusisha na masuala ya watu wenye Ualbino imekabidhi msaada wa nguo,vifaa vya kujifunzia kusoma,kofia za kujikinga na mionzi ya jua na mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Msaada huo uliotolewa na Watu wa nchi ya Israel umekabidhiwa Jumamosi Oktoba 21, 2017 na Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa taasisi ya JTFE, Josephat Torner.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa watoto hao,Torner aliwashukuru Watu wa nchi ya Israel kwa kuguswa na hali ya maisha waliyonayo watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Buhangija.
“Rafiki zangu wa nchini Israel wameniomba nifikishe zawadi hizi kwa watoto hawa wenye wanahitaji mbalimbali,na wameahidi kuendelea kutoa chochote kile kinachoweza kuwafaa watoto hawa”,alieleza Torner.
Naye Msimamizi wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya alisema kituo cha Buhangija hivi kina watoto wenye ualbino 142, watoto wasioona 26 na watoto 60 wasiosikia 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa nguo,kofia,vifaa vya kujifunzia na mafuta yanayozuia mionzi ya jua uliotolewa na Watu wa Israel kwa ajili ya watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akimvalisha nguo mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija.
Mtoto akifurahia baada ya kuvalishwa nguo
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akiendelea na zoezi la kuvalisha nguo watoto
Watoto wakiendelea kuvalishwa nguo
Watoto wakiwa wamevaa nguo kutoka kwa watu wa Israel
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akimvalisha mtoto kofia ya kujikinga na mionzi ya jua
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akiendelea kugawa kofia kwa watoto
Watoto wakiwa wamevaa kofia huku wameshikilia bango kutoka kwa watu wa Israel 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akiwa na watoto
Zoezi la kugawa kofia kwa watoto likiendelea
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akiteta jambo na watoto baada ya kuwagawia kofia za kujikinga na mionzi ya jua
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akigawa vifaa vya kujifunzia kusoma kwa watoto
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akimkabidhi mtoto mafuta ya kuzuia mionzi ya jua
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE),Josephat Torner akiwa na watoto baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na watu wa Israel.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad