HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 26, 2017

ILALA YA WAPIGA MSASA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI KUHUSU MAAMBUKIZI YA UKIMWI



Mkuu wa Idara ya ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Francisca francis Makoye Akizungumza na viongozi wa Madhehebu ya kutoka kata 40 za Manispaa ya Ilala walifika katika mkutano huo, aliye upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo Sheikh Hamisi Mohamed  (Picha na John Luhende.) 



Na. John Luhende 

Mwambawahabari 
Viongozi wa madhehebu ya  Dini katika manispaa ya Ilala  wamepatiwa mafunzo pamoja na kufanya majadiliano kuhusu mchango wao katika  katika mwitikio wa masuala yanayo husu UKIMWI ,kwakuwa wao hukutana na watu wa jaamii zote ili waweze kuwaeleza  na kuwa kumbusha waumini waoku jiepusha na ugonjwa huo.



Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya Dini kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Ilala walio hudumia mkutano huo wakimsikiliza mwezeshaji kwa makini hayupo picha ni (Picha zote na John Luhende.) 


Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo,  mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii usatawi wa jamii Manispaa ya Ilala Francisca Francis Makoye, Amewaeleza  viongozi hao kuwa  haliya maambukizi ya UKIMWI  katika manispaa hiyo kuwa sinzuri na wao kama viongozi wa Dini wanao wajibu wa kuwakumbusha waumini wao kuwa waamifu kwa ndoa zao na vijana  kujitunza,  na kuaachana na ngono uzembe, kusubiri muda wao japo kuna changamoto nyingi katika umri wao.






Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya Dini 

kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Ilala walio hudumia mkutano huo wakimsikiliza mwezeshaji kwa makini hayupo picha ni (Picha zote na John Luhende.) 

Aidha amewakumbusha vijana kutumia vizuri ujana wao na kushinda vishawishi ili kujiepusha na ngono ambayo imeelezwa kuwa ndiyo njia  kuu inayo eneza ugojnwa huo ukilinganisha na njia zingine.

Hata hivo amesema   kamati za kata za kudhibiti UKIMWI  , moja wapo ya majukumu yake ni kupanga na kushirikiana na wananchi na wadau wengine kuhusu mipango ya kupambana na maambukizi, kukuza uelewa  wa wananchi  kuhusu UKIMWI na uwezo wa kiuchumi wa waathiriwa.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa  juhudi zinahitajika kwa kila kiongozi na wanachi kwa ujumla katika kupambana na  janga la UKIMWI katika ngazi ya kata  ili  hatimaye malengo ya 90 90 90ifikapo 2020 ambayo ni asilimia 90 ya WAVIU wana jua haqli ya kuishi na VVU, na asilimia 90 ya waliogundulika na VVU wanapata matibabu ndelevu ya  dawa za kufubaza virusi na asilimia 90 ya watu wote wanapata dawa za kufubaza Virusi watakuwa na kiwango kidogo cha  Virusi.

Naobaadhi ya viongozi walishiriki mkutano huo wameishukuru manispaa hiyo kwa kuandaa mkutano huo kwani umewaogezea uelewa juu ya afya zao na waumininwao , Shekh Indrisa kutoka Majohe ni moja ya viongozi hao, ameishukuru Manispaa ya Ilala kwa kuandaa mkutano huo wa siku mbili  kwani wameweza kuelewa namna serikali inavyo wajali  wanachi wake hasa katika kuwa hudumia kwa kuwapatia dawa na hudumanyingine za kiafya na kuhakikisha usalama wao wakati wote.


“kwakweli kuna jambo moja sizuri sana hasa wawezeshaji walivyo tuelezea kuhusu sheria ya UKIMWI ya 2008 kuhusu watu wanaoeneza ugojwa huu kwa makusudi, naomba watu hao waache kabisa kwa mwenyezi Mungu atawapa hukumu kwa kuwauwa wenzaokwa makusudi” Aalisema shekh huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad