HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 26 October 2017

HALI ILIVYO JIJINI DAR LEO KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Hivi ndivyo  linavyoonekana eneo la Jangwani jijini Dar es salaam mchana huu, baada ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi ya jiji hili.
 Barabara ya Morogoro ikiwa imefungwa katika eneo la Fire, kufuatia maji mengi kujaa katika eneo Jangwani baada ya mvua kubwa ilinyeka maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam leo.
 Vikwangua anga vikiwa vimetandwa na wingu la Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar leo.
 Katika hali kama hii, baadhi ya wakazi wa Dar huona ni fursa kwao kutupa uchafu.
 Mkazi wa jiji la Dar akitota maji baada ya kutowa na mvua inayoendelea kunyesha wakati akisuburi kuvuka barabara katika eneo la Makutano ya Bibi Titi na Morogoro.
Usiombee gari ikubumie kiwese pindi mvua ikiwa inanyesha, maana unaipiga kibega peke yako labda kwa msaada wa abiria.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad