HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 9, 2017

DC Mwanga awaweka ndani Watendaji watatu kwa kosa kuwachangisha wananchi fedha za mafuta

Mkuu wa wilaya ya Mwanga Bw Aron Mbogho awakamata na kuwaweka ndani watendaji watatu wa kituo cha afya cha Kisangara baada ya kuwachangisha wananchi fedha za mafuta ya gari la kubebea wagonjwa utaratibu ulikatazwa na serikali  hatua ambayo pia inadaiwa  kusababisha mgonjwa kufariki akiwa ndani ya gari hilo wakati linasubiri fedha za mafuta.

Akizungumza na ITV Bw.Mbogho amesema kitendo kilichofanywa na watendaji hao hakikubaliki na ni cha makusudi kwani hata kama kulikuwa na tatizo la mafuta ziko njia nyingine ambazo zingeweza kutumika kuwafikisha wagonjwa kwenye tiba na hawakutaka kuutumia.

Wakisimulia mkasa huo baadhi ya ndugu wa mgonjwa aliyepoteza maisha  wamesema siku ya tarehe 5/10/2017. Katika eneo la Kisangara vijana watatu waliokuwa kwenye pikipiki waligongwa na gari majira ya saa 12 jioni na walipofikishwa kwenye kituo cha afya waliandikiwa kwenda KCMC na ndipo wakatakiwa kutoa elfu 50 kwa ajili ya mafuta .

Wamesema pamoja na majeruhi hao kuingizwa kwenye gari la wagonjwa walianza kuzunguka mitaani kuchanga hadi saa tatu usiku wakipopazipata na wakiwa njiani kwenda KCMC mmoja alipoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi.

Diwani wa kata ya Lembeni amesema utaratibu wa kuwataka wananchi kuchangia gharama za mafuta ya gari la wagonjwa ulipitishwa kwenye vikao vyao lakini kwa makubaliano kuwa ufanyike baada ya mgonjwa kufikishwa kwenye matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad