HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 7 October 2017

BENKI YA CRDB TAWI LA KARIAKOO WAWAPA ZAWADI WATEJA MAALUMU PAMOJA NA KUFANYA USAFI KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

Meneja wa benki ya CRDB kwa wateja wadogo na wakati, Jesca Nyachiro akizungumza na wateja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam wakati wakisheherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba. 
Mteja wa benki ya CRDB na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tripple "S" Investment Limited, Geofrey  Rwenyagira akizungumza na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya CRDB tawi la kariakoo jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa akizungumzia changamoto mbalimbali pamoja na mafanikio aliyoyapata. Pia aliwaasa wafanyakazi wa beni hiyo kuvumiliana katika furaha na matatizo mbalimbali ya wateja wake.
Mfanyakazi wa benki ya CRDB makao makuu akifafanua jambo mbele ya wateja na wafanyakazi wa benki ya CRDB katika tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja waliohudhulia katika hafla fupi iliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Kariakoo.
 Mfayakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki  hiyo katika Hafla fupi ya kuwapa zawadi wateja maaalumu wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakiwa katika picha pamoja na wateja waliohudhulia hafla fupi ya kuwashukuru pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali wateja wake.


 Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakiwa katika picha pamoja na wateja waliohudhulia hafla fupi ya kuwashukuru pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali wateja wake.
 Mteja wa benki ya CRDB na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tripple "S" Investment Limited, Geofrey  Rwenyagira akishirikiana na Meneja wa benki ya CRDB kwa wateja wadogo na wakati, Jesca Nyachiro Nyachiro kukata keki kwaajili ya kuwashukuru wateja maalumu wa Tawi la Kariakoo katika wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba.


Meneja wa benki ya CRDB kwa wateja wadogo na wakati, Jesca Nyachiro akiwalisha keki wateja maalumu wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo katika wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba.
Meneja wa benki ya CRDB kwa wateja wadogo na wakati, Jesca Nyachiro akilishwa keki na meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo,Diana Mtalo wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba. 

 meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo,Diana Mtalo akita zawadi kwa wateja wa mda mrefu pamoja na wateja maalumu wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam.Ikiwa ni Kusherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba duniani kote

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo wakifanya usafi maeneo mbalimbali yaliyo karibu na Benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. 
 Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Diana Mtalo akitoam msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad