HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 4, 2017

BENKI YA AZANIA IMEAMUA KWENDA BEGA KWA BEGA KUWATEMBELEA WATEJA WAKE


Na Mwandhishi Wetu
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imeanza kuwatembelea wateja wake katika maeneo yao ya kazi ili kusikiliza kwa ukaribu changamoto wanazokutana nazo zinazohusu  huduma za kibenki, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa kuwa wateja wake.

Aidha, katika wiki hii ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imemtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Azania Bank Limited, Ndugu Charles Jackson Itembe, ambaye pia ameongoza msafara wa kutembelea wateja katika maeneo yao ya kazi, ambapo mteja aliyetembelewa leo na Benki hiyo, Ndugu Augustine Nyato amekabidhiwa hati ya kuthaminiwa pamoja na biashara ya mteja huyo kuwa katika biashara watakazozipa kipaumbele.

Akizungumza na mteja huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe amesema ikiwa Azania Benki inamjali mteja wameamua kuwatembelea wateja wadogo, wa kati na wakubwa ili kuwapa shukrani kwa kuendelea kuwa na wao katika biashara kwa kipindi kirefu na hata kwa kipindi kijacho ili kunafaika na benki hiyo.

Naye Mteja huyo ambaye ni Mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company Augustine Nyato ameishukuru benki ya Azania kwa kutambua mchango mkubwa wa wateja wao mpaka wakaamua kumtembelea ili kusikiliza changamoto anazozipata katika benki hiyo pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana vyema katika kutoa huduma iliyobora ili kufikia malengo aliyojiwekea.

Wiki ya huduma kwa wateja imeanza rasmi Jumatatu ya Oktoba 2, 2017 na itamalizika baada ya wiki moja. Ni wakati wa taasisi kuwa karibu zaidi na wateja wake. Ni wakati wa kwenda bega kwa bega katika kuleta maendeleo kwa taifa letu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akizungumza na mteja wa benki ya Azania ambaye ni mfanyabiashara na mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company  Augustine Nyato kuhusu benki hiyo ilivyoamua kuwatembelea wateja wake katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company Augustine Nyato(katikati) akizungumza kuhusu faida anazozipata pamoja na kuishukuru benki ya Azania kwa kuona umuhimu wa kuwatembelea wateja wao kuwa wanawajali kuliko kubaki maofisini wakisubilia wateja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
 Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati (kulia) akizungumza na mteja wa Benki hiyo kuhusu bidhaa walizonazo kwenye benki hiyo na namna wanavyoweza kushirikiana kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendelea kwa taifa.Kulia ni mteja wa Banki ya Azania, Bwana Augustine Nyato(kushoto).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) akimkabidhi  hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania, Bwana Augustine Nyato leo ofisini kwake katika mtaa wa Survey jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya.
Mteja wa Banki ya Azania bwana Augustine Nyato( wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto), Meneja wa Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya(wa pili kutoa kulia) na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati (kulia).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad