HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 15 October 2017

ASKOFU MKUU WA KANISA LA AICT SILASI KEZAKUBI AFUNGUA PASTORETI MPYA YA KANISA LA AICT MTO JORDAN KAHAMA MJINI

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi leo Jumapili Oktoba 15,2017 amezindua na kufungua Pastoreti mpya ya Kanisa la AICT Mto Yodani lililopo Shunu mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Ibada ya uzinduzi na ufunguzi wa kanisa hilo imehudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga,ambapo askofu Kezakubi pia alihubiri katika Ibada ya Jumapili katika kanisa hilo.
Akizungumza kanisani hapo,Askofu Kezakubi aliwataka viongozi na waumini wa kanisa hilo kutumia jengo hilo kwa ajili a ibada na siyo vinginevyo.
“Nimefungua kanisa hili mlitumie kwa ajili ibada,pia kuwaita watu wengine waje kusikia neno la mungu ,sitaki kusikia mnatumia nyumba hii ya ibada kutukanana na kufanya mambo yasiyompendeza Mungu”,alieleza Askofu Kezakubi.
“Ni aibu kusikia kelele kwenye kanisa,watu kutukanana kwene nyumba ya Mungu,kama kuna mabaraza yanafanyika kanisani basi yafanyike kama ibada,vivyo hivyo upande wa kwaya,sitaki kusikia mtu anatukuzwa kanisani,mwenye kutukuzwa ni Mungu pekee”,aliongeza Askofu Kezakubi.
Katika hatua nyingine alisema mchungaji ndiye mwalimu na msimamizi mkuu wa masuala ya kiroho hivyo kuwataka wachungaji kufanya kazi yao vyema kwa kuepuka kuwa wavivu na kutolegea kuwaombea na kuwatembelea waumini. Askofu Kezakubi alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha baadhi ya watu wanaopinga viongozi wa dini  kwenye makanisa kuacha tabia hiyo kwani wanakwamisha kazi ya Mungu huku akiwataka viongozi na waumini kushikamana katika kumtumikia Mungu. "Kuna watu wapo kwenye makanisa yetu kwa bahati mbaya,wakiingia kanisani wanaanza vita badala ya kuwaunga mkono viongozi wao ili wafanye kazi yao vizuri,wakristo mnatakiwa pia kuwatunza watumishi wa mungu,tuwatunze watu waliolitumikia kanisa kwani tusipowatunza tunakosa baraka",alieleza Askofu Kezakubi. Aidha aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuiombea serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo viovu. "Wakristo mnapaswa kumtii mungu,tuenende katika maisha anayotaka bwana,tusimame imara na kukataa mambo mabaya,kama mtu ataliharibu hekalu la Mungu,Mungu atamharibu mtu huyo",alisema.
Akisoma risala Mwalimu Lucas Matanya alisema Kanisa la AICT Mto Jordani lilianzishwa Novemba 13,2013 chini ya Mwinjilisti Nicodemus Lufega likiwa na wakristo 7 wakisali chini ya mti na baadae idadi iliongezeka kidogo wakajenga banda ambapo waliendelea na ibada katika eneo la Lugela mtaa wa Shunu mjini Kahama.
“Kanisa hili limekuwa tawi la AICT Kahama Mjini na kwa ushirikiano uliopo,walinunua eneo na kuanza kujenga jengo hili la kuabudia na nyumba ya kichungaji,choo na kuweka uzio,lengo likiwa ni kuhakikisha wanapata huduma za kiroho karibu na makazi yao”,alieleza.
Aidha alisema Baraza la Utumaji la Dayosisi ya Shinyanga limemtuma Mchungaji Daudi Kazimoto kuwa mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.
Alizitaja changamoto zinazolikabili kanisa hilo kuwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kununulia eneo ili kupanua eneo la kanisa kwani lililopo ni dogo lakini pia ukosefu wa jengo la utawala.
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akizungumza kabla ya kuzindua kanisa la AICT Mto Jordan leo Jumapili Oktoba 15,2016 mjini Kahama-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waumini wa kanisa la AICT Mto Jordan wakishuhudia zoezi la ufunguzi wa kanisa hilo Mchungaji Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akisoma neno la Mungu wakati wa zoezi la kuzindua kanisa la AICT Mto Jordan Mwalimu Lucas Matanya akisoma risala kuhusu kanisa hilo jipya
Waumini wa kanisa hilo wakishuhudia zoezi la uzinduzi wa kanisa hilo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad