HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 18 October 2017

ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA JACKSON MAYANJA AJIUZULU MWENYEWE

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba  raia wa Uganda Jackson Mayanja ni kwamba ameamua kuachia ngazi kutokana na matatizo yake binafsi.

Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo binafsi na kutapelekea kushindw akutimiza majukumu yake kama kocha msaidizi wa timu hiyo.

Ametanabaisha kuwa matatizo hayo ni ya kifamilia na hataweza kukuyaweja wazi, “Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema.

Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake huku kukiwa na sintofahamu kwa siku za hivi karibuni ndani ya klabu ya Simba ikielezwa kwamba kuna matatizo ya kifedha na ucheleweshwaji wa malipo ya mishahara kwa benchi la ufundi na wachezaji kiujumla.

Taarifa hizo ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa Simba haujathibisha taarifa hizo zinazosambazwa kwa sasa kuwa hawajawalipa wachezaji wao mishahara ya miezi mitatu.

x

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad