HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 25 September 2017

WASHINDI 15 KATI YA 50 WAIBUKA KIDEDEA KATIKA MCHEZO WA GOFU KATIKA MASHINDANO MM GOLF TANZANIA.

WACHEZAJI 15 kati ya 50 wa mchezo wa gofu wa mashindano ya MM Gofu Tanzania ambapo mwishoni mwa wiki walitamatisha mashindano ya Robo fainali waliibuka kidedea baada ya kufanya vizuri katika mashindano  yaliyodhaminiwa
 na Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania yaliyokuwa katika viwanja vya Mchezo wa Gofu, Lugalo jijini Dar es salaam.

Wachezaji walioshinda katika mchezo huo ni Steve Lokono, 
Samweli Miginda, 
Patrick, Karimi, 
Sande Walter, na k
wa upande wa wasaidizi ni Wamungu Wagochochi,  MpT Sheko na Kain Mbaya 

Washindi wa mchezo huo wengine ni Fred Laizer na T. Wiliamu.
Z.Hamis, L. Juma, Karim Rasho na kwa upande wa wanawake (MMS), alikuwa ni Karobia.

 Na kwa upande wa watoto  wakiume mshindi ni Wambugu Wagichochi na mshindi kwa watoto wa kike ni A.Eaton, N.Pin na Kain Mbaya
 na mshindi wa Mitupo Mingi ni Mulani Njeru.


Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Mkurugeanzi Mtendaji wa Kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kutokana na kuwa wadau wakubwa wa michezo nchini pamoja na utoaji huduma ya mafuta na vilainishi vya magari hapa nchini.

Muhato alisema udhamini wao wa mashindano hayo kwa mwaka huu si mwanzo bali wataendelea kuyadhamini kila mwaka ili kuweza kuuendeleza mchezo huo nchini. 

 Wachezaji wa timu Gofu inayoshiriki mashindano ya MM Golf Tanzania, Mashindano yanadhaminiwa na Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania yanayoendelea kwa hatua ya robo fainali, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao, kwenye viwanja vya Mchezo wa Gofu, Lugalo jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2017.
 Mchezaji wa timu Gofu inayoshiriki mashindano ya MM Golf Tanzania yanayoendelea kwa hatua ya robo fainali, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta Engen Tanzania, Paul Muhato akipiga moja ya mitupo katika uliofanyika viwanja vya Mchezo wa Gofu, Lugalo jijini Dar es salaam Septemba 23, 2017. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania.


Mchezaji wa timu Gofu inayoshiriki mashindano ya MM Golf Tanzania yanayoendelea kwa hatua ya robo fainali, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta Engen Tanzania, Paul Muhato akipiga moja ya mitupo katika uliofanyika viwanja vya Mchezo wa Gofu, Lugalo jijini Dar es salaam Septemba 23, 2017. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania.
 Mkurugeanzi Mtendaji wa Kampuni ya Engen Tanzania, Paul Muhato akizungumza kabla ya kutoa zawadi kwa washindi wa mchezo wa Gofu wa mashindano ya MM Golf Tanzania yaliyokuwa wakifanyika katika viwanja vya Gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania.

Washindi wa Mchezo wa Gofu wakipewa zawadi mara baada ya kutangazwa washindi katika mashindalo ya Robo fainali yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya gofu ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad