HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 29, 2017

Vijana wa Temeke wajitokeza kutumia fursa mradi wa MYICD.

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wajitokeza kujiunga  na mradi wa sauti ya vijana MYICD iliyo sajiriwa  mwaka 2009, ikiwa kijana ni nguvu kazi ya Taifa ambapo  wanalenga zaidi umri kuanzia 15-35  na kauli mbiu ni kijana paza sauti.

Katika semina hiyo ya mafunzo yaliyofanyika ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala  kwenye halmashari ya Temeke Jijini Dar es Salaam ikiwa  dhumuni la  mafunzo hayo ni  kujua  namna ya kuunda majukwaa ya vijana kuhamasisha, ushirikiano, muongozo wa vijana katika kisiasa, kiuchumi, kijamii pamoja na kidini.

Pia vijana hao wametakiwa kujitambua katika kupata sauti zao pamoja juu  ya haki na mahitaji yao, kwa kujikusanya na kutoa taarifa shirikishi  juu  ya fursa za kimaendeleo.

Afisa maendeleo kata ya Kilakala, Mwajuma Msafiri amesema kuwa vijana hao wameupokea wito  huo vizuri kwa kuchangamkia fursa  hiyo na wapo bege kwa bega katika kushirikiana na vijana wenzao waishio katika mitaa mitano (5) ya kata hiyo ambayo ni Barabara ya Mwinyi, Igunga, Kilakala, Kiaembe Samaki na Yombo Dovya.

Nae Mkurugenzi Taasisi  ya MYIDC, Ismail Mnikite amesema kuwa katika mradi huo unaohusisha kata nne  za Halmashauri ya Temeke ambazo ni Buza, Makangarawe, Tandika na Kilakala ambapo vijana wa vikundi vya  mbio za pole pole ndio waliojitokeza  kujiunga na mradi ili   kupata mafunzo yanayowajenga katika kuleta maendeleo hapa Nchini, vile vile ametoa shukrani za dhati Kwa wiongozi wa Halmashauri hiyo Kwa kuonyesha ushirikiano juu ya Swala hilo.
 Mkurugenzi Taasisi MYICD, Ismail Mnikite akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo ulisajiriwa mwaka 2009 ikiwa ni dhumuni  la  kuinua vijana katika kuwanchinimafunzo na fursa mbalimbali katika kuleta   maendeleo katika ofisi ya mtendaji kata ya kilakala  Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
 Afisa maendeleo kata ya Kilakala, Mwajuma Msafiri akizungumza na waandishi wa habari   kuhusu muamko wa vijana kujitokeza kujiunga na kupata mafunzo yanayotolewa mradi wa MYICD Kwa lengo la  kutaka kuleta mapinduzi  na maendeleo hapa nchini katika ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa mradi, Kassonga Mario akitoa mafunzo kwa vijana hao katika ukumbi wa ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam. 
Vijana wa kata ya kilakala waliojitokeza kwenye mafunzo katika Ukumbi wa ofisi ya mtendaji kata ya Kilakala halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam yalioandaliwa na mradi wa MYICD ikiwa lengo ni kutaka kupaza sauti za vijana. Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad