HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 8, 2017

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUTUMIA MUDA VIZURI ILI KUFIKIA MALENGO WALIYOJIWEKEA

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimvisha taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akimpongeza Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo kwa ushindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini leo mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akipokea nyaraka za ushindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini kutoka kwa mshindi wa taji hilo Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini Dodoma.
 Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura. 
Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo. (Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura amewataka vijana nchini kutumia muda vizuri na mazingira yanayowazunguka ili kufikia azma ya malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri Wambura ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipokuwa akimpongeza Mlimbwende Witness Teddy Kavumo ambaye ni Mtanzania anayeishi Afrika Kusini kwa kushinda taji la Miss Garden Route 2017/2018  Mei 6 mwaka huu nchini humo katika mji wa George.

Mlimbwnde Witness aliibuka mshindi wa Miss Garden Route 2017/2018 akiwa ni miongoni mwa washindani 14 walioingia fainali baada ya mchujo wa awali wa washiriki 600.

“Ni dhahiri umetumia ujuzi, ubunifu, sanaa, imani, bidii, desturi, maadili, na sheria ambavyo umevipata  kutoka kwa familia, jamii ya Kitanzania na pia kwa jamii ya watu wa  Afrika Kusini” amesema Naibu Waziri Wambura.

“Vijana wa Kitanzania, Mlimbwende Witness Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017 la Afrika Kusini amewaonesha njia, mjenge utamaduni wa kupambana na mazingira ili kufikia azma mnazojiwekea” alisistiza Naibu Waziri Wambura.
Aidha, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Bi Witness ameonesha uzalendo kwa nchi yake kwa kuamua kuja Dodoma na kutoa taarifa ya mafanikio yake kama Mtanzania kwa ushindi alioupata katika mashindano ya ubunifu mavazi huko Afrika ya Kusini.
Hatua hiyo inaonesha Mlimbwende huyo ameumeuthamini Utanzania wake na kuonesha kujali kutumia muda wa ziada kwa masuala ya fani ya urembo licha ya kwamba jukumu lake la msingi nchini humo ni la Kimasomo.
Zaidi ya hayo Naibu Waziri Wambura amesema kuwa fani ya ubunifu na mitindo inatambulisha utamaduni, kuongeza kipato, kuinua uchumi na kukuza utalii kwa kuongeza juhudi, maarifa na kufanya kazi kwa bidii hatua nambayo inaleta matokeo mazuri yenye tija.

Aidha, Naibu Waziri Wambura amemshauri Witness, kutumia bidhaa zenye asili ya Tanzania katika fani yake, ili kuzitangaza katika soko la ndani na la nje, kuvutia utalii, kuingiza kipato na  kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo kwake yeye binafsi na kwa Taifa.
Kwa upande wake Miss Garden Route 2017/2018 Mlimbwende Witness amesema kuwa anajivunia kuwa Mtanzania na kuonesha uzalendo kwa nchi yake na amewashauri Watanzania kusimama kwa kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mashindano ya Miss Garden Route 2017/2018 yaliandaliwa na ‘The RoleModels Foundation” kwa kushirikiana na Wakala wengine akiwemo “Gemini Modelling Agency” iliyopo Mossel Bay  Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad