HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 13, 2017

UTAFITI: KIWANGO CHA NIKOTINI KINACHOPATIKANA KWENYE ASALI HAKINA UWEZO WA KUDHURU MWILI WA BINADAMU

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa ripoti ya tafiti ya asali zilizokusanywa zenye chembechembe za nikotini kuwa zimefanyiwa majaribio na  zimedhihirisha kuwa chembechembe  hizo ni chache sana na hazina uwezo wa  kudhuru mwili wa binadamu.

Akizungumza na Vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Glory Mziray amesema  TFS wamekuwa wakukisanya sampuli kila baada ya miaka miwili  kutoka kwa wafugaji nyuki na kuzipeleka kwenye  Maabara za kimataifa na mara zote  zimekutwa zikiwa na ubora wa hali ya juu unaokidhi masoko yote ya kitaifa na kimataifa.

Amezitaja tafiti  mbili zilizofanyika mwaka 2016 kuwa  lengo lake lilikuwa ni kuainisha madhara ya  ufugaji nyuki kwenye maeneo yanayolima Tumbaku na ameyataja maeneo yaliyofanyiwa utafiti huo kuwa  ni mkoa wa Tabora na Kigoma

Mziray  amesema tafiti hizo zimebainisha kuwa kiwango cha nikotini kinachopatikana  kwenye asali iliyochavushwa katika mikoa inayolima Tumbaku ni sawa na nikotini iliyopatikana kwenye asali  ilivyochavushwa na mimea mingine kama vile  nyanya na miombo hivyo kiwango hicho cha nikotini hakina madhara kwa binadamu.


Amesema  watumiaji wa asali wamekuwa wakihukumu uwepo wa nikotini   kwenye asali kwa kuangalia rangi ya asali sambamba na uchungu wa asali lakini asali za Tanzania zinatengenezwa kwa mchanganyiko wa maua ya mimea mbalimbali  jambo ambalo linathibitishwa si nikotini peke yake ndiyo inasababisha uchungu bali mimea mingine kama vile muarobaini. 

Mziray amewataka watumiaji wa asali kuendelea kuitumia kwa vile  asali ni chakula cha kiasili kinachotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mimea mbalimbali.

Ameongeza kuwa, asali ni mchanganyiko uliotokana na maji, Sukari (fruktosi, glukosi, sakrosi) madini pamoja na vitamin.
Baadhi ya Sampuli ya asali inayopatikana katika maeneo mbalimbali za nchi. Asali hutumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad