HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 21 September 2017

UMOJA WA MASOKO MKOA WA DAR ES SALAAM WACHANGIA VYAKULA KWA AJILI YA WAFYATUAJI TOFALI.

 Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Mwajuma Magwiza akipokea msaada vya vyakula kutoka kwa Mwenyekiti wa MUMADA, Mohamed Mwekya ikiwa kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ujenzi wa ofisi za walimu.MUUNGANO wa Umoja wa Masoko ya Mkoa wa Dar es Salaam (MUMADA) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mohamed Mwekya wamekabidhi kilo za mchele 2835, Kilo 600 za Maharage pamoja Chumvi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ujenzi wa ofisi za walimu.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mwenyekiti wa MUMADA, Mwekya amesema kuwa wao kama wafanyabishara wameguswa na harakati za RC Makonda katika kuboresha elimu hususani mazingira ya walimu, hivyo wameamua kutoa mchango wao huo ambao wana imani utasaidia.

Mwekya amesema wataendelea kushirikiana na na serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwataka wadau wengine wa maendeleo waunge mkono jitihada hizo zenye lengo ya kuboresha elimu kwa walimu kukaa ofisi zenye hadhi na taaluma yao.

Nae Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Mwajuma Magwiza amesema kuwa mchango huo utakwenda kwa shughuli iliyokusudiwa na wana imani kila mmoja akijitolea watatimiza lengo la kujenga ofisi 19 za walimu katika wilaya ya Kinondoni.

 Sehemu ya msaada vyakula kwa ajili ya watu wataofyatua tofali kwa ajili ya ujenzi ofisi za walimu.

.Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana, Mwajuma Magwiza akiwa katika ya pamoja na Muungano wa Umoja wa Masoko ya Mkoa wa Dar es Salaam (MUMADA) leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad