HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 10, 2017

Tigo yaja na Twende App kuwawezesha wasafiri kupata huduma ya usafiri kupitia simu za mkonon

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) na Mkurugenzi wa Twende App Justin Kashaigili (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma mpya ya simu za mkononi ijulikanayo kama Twende App inayiowawezesha wasari kupata huduma ya haraka na usalama ya usafiri wa umma wa Taxi, pikipiki za bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu kwa kutumia simu za mkononi.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeungana na kampni inayotoa huduma za usafiri Twende App kuzindua huduma mpya itakayowezehsa wasafiri kupata huduma bora, ya haraka na uhakika zaidi kupitia mfumo wa simu za mkononi unaojulikana kama Twende App.

TwendeApp ni mfumo wa kidigitali wa simu za mkononi unaowezesha wasafiri kutafuta na kupata usafiri wa taxi, pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda) na zile za magurudumu matatu kupitia simu zao za mkononi kwa uhakika zaidi na kwa bei nafuu.

Twende App ambayo, tayari inatumika katika jiji la Dar es salaam, sasa imepanua wigo wake na kufikia miji ya Arusha, Morogoro, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma Iringa na Mbeya. Kuna mipango ya kusambaza huduma hiyo kwenda Zanzibar, Tanga na Mtwara.

Akizungumza katika uzinduzi wa Wende App jijini Arusha leo, Meneja Uhusiano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Twende App inatumia teknologia ya GPS kwa kutegemea mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo. Hii inawahakikishia watumiaji huduma ya uhakika, haraka na yenye usalama wa hali ya juu.

‘Kwa sasa magari mengi ya usafiri wa taxi na bodaboda yamepaki kwenye vijiwe wakisubiri wateja. Twende App itawaunganisha madereva na wasafiri kwa muda na sehemu sahihi na inayohitajika. Kwa kupakua mfumio wa Twende App kwenye simu zao za mkononi, wasafiri wataweza kuwasiliana kwa haraka na madereva wa vyombo vya usafiri wa umma ambao wapo karibu zaidi na eneo husika ambapo usafiri wenyewe unahitajika. Hii inaondoa adha ya kutembea kutafuta usafiri na pia inapunguza muda wa kusubiri usafiri kwani mteja anawasiliana kwa haraka na chombo cha usafiri kilichokuwa karibu zaidi naye. Kwa upande wa madereva, Twende App itawaokolea muda, kuwaongezea wateja na kuongeza mapato kwa kuwa hawahitaji tena kushinda kijiweni wakisubiri wateja,’ alisema.

‘Wateja wanaohitaji usafiri wanaweza kuona eneo ambalo madereva wapo kwa kutumia teknologia ya GPS na mfumo wa Google maps. Baada ya hapa watatuma ombi la kupata usafiri na moja kwa moja, mtandao huu wa Twende App utamjulisha dereva aliye karibu zaidi kuhusu ombi hili la usafiri na eneo ambalo msafiri yupo,’aliongeza.

Woinde aliongeza kuwa mfumo huu wa kisasa unapatikana kupitia simu za kisasa za kupangusa (smartphones), kwa hiyo utaongeza matumizi ya simu za kisasa nchini ikiwemo matumizi ya mfumo wa kutumia simu za mkononi kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa mbali mbali.

‘Twende App pia inakuletea matumizi ya Tigo pesa katika biashara ya usafiri. Hii inaendana na dhana kuu ya Tigo ambayo ni kuongeza matumizi ya mfumo wa digitali nchini pamoja na kutoa huduma ambazo zinaboresha na kujibu mahitajiya wateja wake nchini kote. Tunawaasa wateja wetu kujaribu mfumo huu mpya katika kipindi hiki cha Tigo Fiesta 2017 kama njia bora ya kwenda na kutoka kwenye matamasha ya msimu huu,’ Woinde alisema.

Mkurugenzi wa Twende App, Justin Kashaigili, alisema kuwa mfumo huu unatumia madereva na magari ambayo yana leseni halali za udereva na za biashara, na waliothibitishwa kutokuwa na historia ya uhalifu. Hii inawahakikishia wasafiri usalama wao. Kwa kushirikiana na Tigo, Twende App pia inatoa simu za kisasa zaidi ya 1,000 kwa madereva wanaojisajili na Twende App ili kuwawezesha madereva kufanya biashara zao kwa umakini zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Taxi wa Arusha, Ali Mohammed, aliusifu mfumo huo mpya huku akisema kuwa utawaongezea kipato, usalama na kuwapa uhakika zaidi katika biashara zao.

‘Kwa bahati mbaya kumekuwa na matukio ya uhalifu yanayohusu madereva na hata abiria wa usafiri wa umma. Twende App itasaidia kuondoa hofu baina ya dereva na msafiri kwani wote wanakuwa wamesajiliwa katika mfumo mmoja kwa hiyo hata upotevu wa aina yoyote ukitokea, suala la ufuatiliaji linakuwa rahisi,’ alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad