HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 13, 2017

TFF YATOA MIPIRA 300 KWA VITUO VYA KUKUZIA SOKA LA VIJANA JIJINI DAR ES SALAAM


Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Nyambaya akizungumza na waandishi wa habari na viongozi wa wilaya kabla ya kukabidhi mipira kwa ajili ya kuwapatia viongozi wenye vituo vya kukuza vipaji vya mpira, kushoto ni makamu mwenyekiti wa chama cha soka Dar es salaam (DRFA) Salum Mwaking'inda.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa mipira 300 kwa viongozi wa vituo na wilaya katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mpango wa kuinua soka la vijana.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda ya Dar es Salaam na makamu mwenyekiti wa soka la Vijana Lameck Nyambaya amekabidhi mipira hiyo kwa lengo la vituo vinavyopatikana jiji la Dar es Saaalm kuweza kuwasaidia na pia kuona soka la vijana linafanikiwa.

Nyambaya alisema TFF watahakikisha mipira hiyo inatumika vizuri ili kutimiza lengo la kuibua na kuwa na vipaji vingi vya mpira ambavyo watakuja kuwa msaada kwa timu za vijana na timu ya taifa. 

"Tunaigawa mipira hii kwa vituo vya soka na mimi binafsi nitahakikisha kunakuwa na matumizi sahihi na sio vinginevyo.

Kutokana na ukubwa wa jijini hili, nilimuomba Rais wa TFF atupatie mipira 200 ambayo ametupatia na mimi mwenyewe nitaongeza mipira 100," alisema Nyambaya.

Hivi karibuni, TFF ilianzisha kampeni ya kugawa jumla ya mipira 3,100 ya soka nchi nzima kwa ajili ya soka la vijana.

Mipira hiyo imekabidhiwa kwa viongozi wa wilaya za Kinondoni, Ilala, Temeke, Kigamboni na Ubumgo.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda ya Dar es Salaam na Lameck Nyambaya akikabidhi mpira kwa Makamu Mwenyekiti
wa chama cha soka Dar es salaam (DRFA) Salum Mwaking'inda

na kuwakabidhi viongozi wa wilaya 
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Nyambaya akiwa anachezea moja ya mipira aliyokabidhi leo kwa viongozi wa wilaya za Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad