HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 21, 2017

SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye eneo la uwekaji jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha, Septemba 21, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea kirungu ikiwa ni zawadi ya asili ya Kabila la Wamasai kutoka   kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya Longido, Thomas Olengulupa  kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea usinga  ikiwa ni zawadi ya asili ya Kabila la Wamasai kutoka  kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya Longido, Thomas Olengulupa  kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Longido kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha Septemba 21,  2017. 
 Baadhi ya Wananchi wa Longido wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa wakati alipozungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha, Septemba 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka  jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama wilayani Longido mkoani Arusha kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 15.8. 

Waziri Mkuu ameweka jiwe hilo la msingi leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji  wa Longido Mjini pamoja na kijiji cha Oltepesi  ambao chanzo chake ni kutoka mto Simba wilaya ya Hai mkoani Kilimanajro.
Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kupeleta wataalamu wilayani Longido ambao watashirikiana na Halmashuri za wilaya ya Longido na tarafa ya  Loliondo  kutafuta vyanzo vingine vya maji ili wananchi waweze kupata maji  ya kutosha.

Waziri Mkuu amesema asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya za Longido na Ngorongoro ni wafungaji hivyo wanahitaji maji mengi watakayoyatumia katika matumizi yao ya kawaida ya nyumbani pamoja na kunyweshea migugo.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo pamoja na miradi mingine midogo tisa katika wilaya ya Longido kutumia vifaa vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia viwanda.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.

Awali Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Lwenge aliwaagiza Wakandarasi wanaojenga mradi huo kuhakikisha wanajenga kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyohitajika pamoja na kumaliza kwa wakati. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2018.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
ALHAMISI, SEPTEMBA 21, 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad