HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 12, 2017

RAIS DKT MAGUFULI AMJULIA HALI MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA ALIYEJERUHIWA KWA RISASI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe wakiangalia majeraha aliyopata Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Septemba, 2017 ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen. Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Meja Jen. Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.
Meja Jen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumjulia hali    na kumuombea dua ili apone haraka.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen. Venance Mabeyo pia ametembelea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.
Mhe. Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya Jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine                           na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba akielezea alivyoshambuliwa kwa  risasi mkononi, tumboni na mguuni  wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) wakioneshwa na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Brigedia baadhi ya risasi  zilizotolewa kwenye mwili wa  Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba  baada ya kushambuliwa wakati akiingia  nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe,  Brigedia Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba na wauguzi wakiomba dua wakiongozwa na Mama Margareth Vicent Mritaba hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa Meja Jenerali Mritaba akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto Nathan Martin  wakati akitoka kumjulia hali Meja jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni  wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu  Aloys Konolipa wa Shule ya Msingi Kidugalo wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani alipopita kuwapa pole wagonjwa wengine baada ya kumjulia hali Meja  Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni. Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad