HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 26, 2017

NHIF YAHIMIZA WANAMICHEZO KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA

MFUKO wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewahimiza wana michezo nchini kuchangamkia fursa ya kujiunga na mpango wa matibabu kupitia  mfuko wa afya ya jamii (CHF) na mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu pindi wanapoumia wakiwa michezoni.

Rai hiyo imetolewa  mwishoni mwa wiki na meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Ruvuma Abdiel Mkaro wakati wa Bonanza maalum la kuhamasisha jamii hususana wana michezo kujiunga na mfuko huo na kushiriki mazoea mara kwa mara ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa yasiokuwa ya lazima.

Aliwataka wana michezo na jamii ya watanzania wakiwemo waandishi wa habari,kuona umuhimu wa kijunga na mpango huo  kwa lengo la kuwa na uhakika wa matibabu  pale  inapotokea kupata ajali na magonjwa ya kawaida.

Bonanza hilo liliandaliwa na NHIF lilishirikisha michezo mbalimbali kama vile kukimbia,mazoezi ya viungo,kukimbiza kuku pamoja na mpira wa miguu ambap timu ya soka ya Mkambi FC ilifanikiwa kuibuka mshindi  baada ya kuifunga timu ya NHIF 4-2 kwa njia ya Penalti kufuatia matokeo ya kufungana 1-1 ndani ya Dkt 90 za mchezo huo.

Hata hivyo Bonanza hilo lililoonekana kuvutia watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya manispaa ya Songea, baadhi ya washiriki  wameiomba Nhif kuendelea kuandaa bonanza kama hilo kila mwiso wa mwezi ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki na kufanya mazoezi ili kuepusha uwezekano wa kupata magonjwa.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF mkoa wa Ruvuma Abdiel Mkaro akikagua timu ya Soko ya NHIF wakati wa Bonanza maalum la kuhaamsisha wana michezo mkoa wa Ruvuma kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu pindi wanapoumia.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Ruvuma Abdiel Mkaro kulia akikagua timu ya soka ya Makambi FC kabla ya kuanza mchezo kati ya timu hiyo na timu ya NHIF katika Bonanza la kuhamasisha wana michezo kujiunga na mfuko huo.
Baadhi ya wafanyakzi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoa wa Ruvuma wakizunguka uwanja wa shule ya msingi Mkambi katika manispaa ya Songea wakati wa Bonanza maalum la kuhamasisha wana michezo kujiunga na mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu pale wanapougua.
Wafanyakazi wa NHIF mkoa wa Ruvuma Wakifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la kuhamasisha wanamichezo na jamii kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na mfuko wa afya ya Jamii CHF.
Wafanyakazi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoa wa Ruvuma Salah Kalolo kulia na Edwina Bilungi wakishindana kukimbiza kuku katika Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Makambi Songea mwishoni mwa wiki.

Meneja wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoa wa Ruvuma Abdiel Mkaro akikabidhi zawadi kwa msindi wa mbio za kukimbiza kuku Edwina Bilungi kulia katika Bonanza hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad