Mtaa Kwa Mtaa Blog

MVUTANO WAIBUKA KWENYE BARAZA LA MADIWANI HANDENI KUGOMBEA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA.

Kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Handeni nusura kivunjike baada ya kuibuka hoja inayohusu kujengwa kwa makao makuu ya wilaya kati ya mji mdogo wa Mkata au Kabuku hali ambayo ilibidi busara zitumike ili kikao kiendelee.

Hoja hiyo ambayo iliwasilishwa na diwani wa kata ya Mkata Mh Musa Mwanyumbu huku akimtuhumu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuwa anapendelea upande mmoja.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alikanusha madai hayo na kusema kuwa hajawai kupendelea upande wowote huku mkurugenzi wa halmashauri hiyo akisema kwamba maamuzi ya kujengwa kwa makao makuu ya halmashauri hiyo wanayo madiwani wenyewe.

Kufuatia hatua hiyo baadhi ya madiwani wameomba kama kuna vyombo vya juu vinavyohusika na jambo hilikufika ili kuliweka sawa jambo hili.\

Chanzo: ITV Tanzania

Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget