HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 8 September 2017

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI AGOSTI 2017 UMEPUNGUA-NBS


Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusianaMfumuko wa bei wa Mwezi Agosti Mwaka huu(2017) kwa kipimo cha Mwezi umepungua kwa asilimia 0.4

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti Mwaka huu.Kulia ni Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti 2017 umepungua zaidi hadi kufikia asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Julai2017.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema hii inamanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai,2017.

Kwesigabo alisema Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za Vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 8.6 kutoka asilimia 8.9 ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.

"Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.46 mwezi Agosti, 2017 kutoka 103.28 mwezi Agosti, 2016" alisema Kwesigabo.

Akizungumzia mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Agosti,2017 umepungua hadi asimilia 9.1 kutoka asilimia 9.3 mwezi Julai 2017. Ambapo badiliko la Fahirisi za bei zisizo za vyakula umebaki kuwa asilimia 3.1 mwezi Agosti, 2017 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.

Kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.2 Julai, 2017.

Fahirisi inayotumika kukokota aina hii ya mfumuko wa bei haijumuishi vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani, vinywaji baridi, petroli, dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa kuni na umeme.

Amesema vyakula na bidhaa za nishati vinasifa ya kuwa na bei ambazo hubadilika mara kwa mara, hivyo vikiondolewa kwenye fahirisi ya bidhaa na huduma zote hubakia fahirisi ambayo ina mwelekeo imara kwa watunga sera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad