HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 4, 2017

,MCHENGA BBALL STARS MABINGWA WAPYA WA SPRITE BBALL KINGS 2017

Mabingwa wa Michuano ya Sprite BBall Kings  Mchenga BBall Stars wakiwa pamoja na Afisa Masoko msaidizi wa kampuni ya Coca-Cola Pamela Lugenge (aliyevaa t-shirt ya kijani) baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha Shilingi Milioni 10 sambamba na kukabidhiwa kikomne baada ya kushinda katika mchezo wa fainali uliomalizika kwa Mchenga kushinda kwa pointi 104-94 dhidi ya TMT..



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

TIMU ya Mchenga BBall Stars wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Sprite BBall Kings 2017 baada ya kuibugiza wapinzani wao TMT kwa pointi 104-94 katika fainali ya mwisho iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye Viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es salaam.

Mchenga wanakuwa mabingwa wa Kwanza wa michuano hiyo wakijinyakulia kitita cha shilingi Milioni 10 sambamba na kombe huku TMT ikijinyakulia milioni tatu baada ya kushika nafasi ya pili.

Katika mchezo wa kwanza hadi wanne TMT walifanikiwa kushinda mara mbili sawa na Mchenga na kupelekea mchezo wa tano kuwa wa kasi na ushindani huku kila upande akijaribu kutokufanya makosa na kuibuka kidedea.

Pamoja na hayo, mechi ya leo iliweze kuonyesha utofauti na ufundi mkubwa kutokana na timu zote mbili kupania kuwa bingwa jambo ambalo lilipelekea timu hizo kujikuta zikitoka sare ya pointi 84-84 kwa mara ya kwanza na kupelekea waamuzi kulazimika kuongeza dakika nyingine tano ili aweze kupatikana mshindi wa mashindano hayo na ndipo Mchenga BBall Stars alipomchapa TMT jumla ya pointi 102-94

Timu ya TMT ikiwa imeshikilia mfano wa hundi yenye thamani ya Milioni tatu baada ya kushinda nafasi ya pili michuano ya Sprite BBall Kings 2017.


Kwa upande mwingine, mchezaji Rwahabura Munyagi kutoka timu ya Mchenga BBall Stars ameweza kushinda nafasi ya mchezaji bora 'MVP' kwa kuweza kuipigania timu yake kushinda mchezo wa leo.

 Afisa Masoko msaidizi wa kampuni ya Coca-Cola Pamela Lugenge aliweza kuwakabidhi mabingwa hao wapya wa Sprite BBall Kings 2017 mfano wa hundi ya kiasi cha Milioni 10 pamona na kombe, aliweza pia kuwakabidhi Timu ya TMT na mchezaji bora wa mashindano hayo 'MVP' Rwahabura Munyagi kutoka Mchenga.

Mratibu wa Mashindano hayo, Basilisa Biseko ameweza kuipongeza timu ya Mchenga kwa ushindi huo walioupata wakiwa ndio mabingwa wa kwanza wa Sprite BBall Kings na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa mpira wa kikapu mtaani ili kuweza kuhamasisha watoto na vijana kuupenda mchezo huo na kurejesha thamani ya Mpira wa Kikapu.

Amesema Mwitikio mkubwa wa watu umeonekana katika mashindano hayo hasa katika michezo iliyokuwa inachezwa kwenye Viwanja vya Don Bosco na anaamini mwakani yatakuwa na hamasa zaidi tofauti na mwaka huu.

Mashindano hayo yalianza rasmi mwezi Mei mwaka huu kwa kuanza kufanya usaili kwa timu 54 katika Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam zikianza kwa mtoano kwenye Viwanja mbalimbali na kuhitimishwa wikiendi hii ya Septemba 02.
 Mchezaji bora 'MVP' wa michuano ya Sprite BBall Kings kwa mwaka 2017. Rwahabura Munyagi akiwa ameshikilia kikombe chake sambamba na kupata kiasi cha shilingi Milioni 2.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad