HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 26 September 2017

Mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Tatu Afrika Kushirikisha Nchi sita.

Na Mwandishi wetu.
RWANDA na Sudani zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19 -21.

Nchi hizo mbili zinaungana na nchi nyingine sita zilizothibitisha kufanya hivyo awali kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Chama Cha kuogelea nchini (TSA), Leena Kapadia.

Kapadia amezitaja nchi hizo kuwa ni Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Djibouti na wenyeji Tanzania.

Kapadia amesema kuwa bado wametoa nafasi kwa nchi nyingine kuthibitisha kushiriki hadi wiki moja kabla ya mashindano ili kuleta mvuto na ushindani zaidi. 

“Tumezipa nafasi zaidi kutafuta fedha ili kushiriki, tutafunga mlango wa kuthibitisha wiki moja kabla ya mashindano,” alisema Kapadia.
Alisema kuwa  TSA bado inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanisha mashindano hayo na mpaka sasa kampuni za simu ya Vodacom Tanzania imethibitisha kudhamini mashindao hayo kama wadhamini wakuu.
Kampuni hiyo itagharimia medali na vikombe.

 Wadhamini wengine ni JCDecaux (billboards), Label Promotions (billboards), Print Galore na Slipway Hotel.
Pia kampuni ya ndege ya Swissair imejithibitisha kudhamini tiketi za ndege za waogeleaji wa Tanzania ambao wanasoma nchini Uingereza ambao wapo kwenye timu ya Taifa. Waogeleaji hao ni Sonia Tumiotto, Smriti Gokarn, Anjani Taylor, Collins Saliboko, Natalie Sanford na Marin De Villard. 
Alisema kuwa Tanzania itashirikisha waogeleaji 60 wakigawanywa kwa timu mbili (Tanzania A na B) chini ya makocha wao, Alex Mwaipasi na Michael Livingstone.

Nchi ambazo zimeongezewa muda wa kuthibitisha kushiriki katika mashindano ni Ethiopia, Eritrea, Somalia, Sudani Kusini ambazi zipo kanda ya tatu na za kanda ya nne ni Angola, Botswana, Comoro, Madagascar, Lesotho, Malawi, Mauritius, Seychelles, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na Swaziland.

Alisema kuwa kwa kamati yao inatafuta wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo. Wanahitaji kiasi cha Sh 100 milioni ili kufanya mashindano hayo kwa hadhi inayostahili.
Alisema kuwa wanatarajia waogeleaji zaidi ya 200 kushiriki katika mashindano hayo ambayo Tanzania ni mabingwa watetezi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad