HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 20, 2017

MAKOCHA VIJANA, WANAVYOFUNGUA AKILI ZA WAPENZI WA SOKA DUNIANI.

André Villas-Boas


Na. Honorius Mpangala.
Mwalimu ni fani pana ambayo imekuwa na majina tofauti mengi ambayo hutumika katika kitendo cha kufundisha.Licha ya kuwa kama jina la fani ya kuhawilisha maarifa toka kwa anayejua kwenda kwa asiyejua. Ila yapo majina mengi katika nyanja nyingi ambayo hutumika katika matendo hayo ya kuhawilisha maarifa.

Wako walimu wa mambo mbalimbali,pia kwavile wafanyao kazi hizo ni binadamu basi changamoto hutoke pia. 

Katika mchezo wa soka kuna kocha ambaye hufanya kazi hiyo ya kufundisha wachezaji. Kwa miaka mingi fani hii ya ualimu wa soka ilichukuliwa kama fani ambayo wanaoweza kuitenda vyema ni wale waliocheza soka kwa madaraja ya Juu. 

Lakini kwa kadiri miaka ilivyoweza kusogea mapinduzi ya dhana hiyo yalianza kutoweka taratibu baada ya kuona wako makocha ambao wanafanya vyema pasipo hata kucheza madaraja ya juu katika soka. Wako makocha ambao wametoa mafanikio kwa vilabu vikubwa wakati wao wamecheza katika madaraja ya chini.

Katika ulimwengu wa soka imekuja kuonekana,kucheza soka ni kama kitu cha nyongeza kwa kocha lakini kitu muhimu ni kuweza kufundisha soka. Kutokana na dhana hiyo tumeweza kuwaona makocha wengi vijana wakifanya vyema katika vilabu tofauti duniani. Kuonekana kwao kunafanya kuondoa ile dhana ya awali kuwa ili uwe kocha mzuri lazima upitie katika kusakata soka katika madaraja ya juu.

Alikuwa Jose Mourinho aliyewashangaza wapenzi wengi wa soka kwa Kutokana na kutocheza soka katika madaraja yanayotambulika katika mashindano. Alitazama fursa aliona kama anaweza kuwa mzuri kwa kusoma ualimu wa soka kuliko kujikita na kucheza ilihali kipaji cha kucheza hakikuwa kikubwa cha kumfanya aonekane ni bora mbele ya wenzake.

Wakati yeye Jose akichagua njia hiyo kupita klabu tofauti kama FC Barcelona. Alirejea Ureno na kumfanya Hata kijana mdogo kabisa Andres Villas-Boaz kufuata nyayo zake. AVB alisoma ukocha pasipo kucheza soka katika madaraja makubwa yanayojulikana katika soka la Ureno.

Wakati wadau wengi wanajua Fc Porto ndiyo iliyomtambulisha Mourinho,lakini aliwahi fundisha klabu kama Benfica akiwa kocha mkuu pia. Ilikuwa ni Fc Porto pia iliyoufahamisha umma kuwa wana kocha kijana mwingine tena. Bali hiyo ilizidi kuchochea mapinduzi ya soka kwa Vijana kujikita katika ualimu wa soka licha ya kutokucheza katika madaraja ya juu.

Katika nyakati hizi wako makocha ambao wanazidi kuujuza umma kuwa sio lazima ucheze soka katika daraja la kuu ndipo uweze kuwa kocha mzuri.Pia wapo wachezaji ambao wanacheza huku wakipata mafunzo ya ukocha kwa wakati huohuo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wachezaji kama Ryan Giggs na hata Juma Kaseja . Wakiwa wanacheza wakalazimika kupata mafunzo hayo na kujiandaa kwa maisha ya baadae nje ya kucheza soka lenyewe.

Mohammed Kijuso

Katika klabu ya Mbeya City kwa muda mrefu Mara tu ya kuondoka kocha msaidizi Maka Mwalwisi waliamua kumpa jukumu lile aliyekuwa mchezaji wao Mohammed Kijuso.Akiwa kama kocha msaaidizi alifanya kazi na Juma Mwambusi kama kocha mkuu na baadae Kufanya kazi na Kinnah Phiri. Kwasasa baada ya klabu kuachana na kinnah Phiri majukumu yanakabidhiwa kwa Kijuso.

Akiwa na umri wa miaka 38, usije ukashangaa matokeo bora uwanjani yakawafanya halmashauri ya jiji la Mbeya kuamua kumpa jukumu la kocha wa klabu.Japo Kijuso amecheza soka katika daraja la juu kabisa kwa Tanzania lakini umri wake unamfanya aonekane kocha kijana na kubeba majukumu katika klabu yenye mashabiki wenye ushawishi mkubwa katika klabu yao.

Nyakati zote umri hauwezi kuwa kikwazo kwa watu waliopata maarifa ya kazi waifanyayo kwa umaridadi mkubwa. 

Ligi ya bundesliga iliingia katika historia ya moja ya klabu zake kuongozwa na kocha kijana.Ni oktoba 27,2015 pale klabu ya 1899 TSG Hoffenheim ilipomtangaza kocha wao Julian Nagelsmann. Akiwa na umri wa miaka 28 wapenzi wengi walishikwa na bumbuwazi kwa kuhoji ni wapi alikopita kiuchezaji.
Jose Mourinho

Nagelsmann ni kama ilivyo kwa AVB na Mourinho ni watu walipata maarifa na kufanya vyema darasani na hatuelekeoa vitendo kwa kufundisha soka vyema. Alimua kujiunga kupata mafunzo ya ukocha baada ya kupata majeraha ya goti akiwa akichezea klabu ya Augsburg xhini ya mika 19 akaamua kubadili uelekeo.
Hadi sasa Mjerumani huyo wa Hoffenheim ana umri wa Miaka 30. Akiwa amepita katika ngazi tofauti za ufundishaji wa soka kwa kuanzia ngazi ya chini ya miaka 17 kwa baadhi ya klabu.

Nagelsmann ni msomi pia kiwango cha shahada katika masuala ya uongozi katika biashara na pia mtaalamu wa Sayansi ya Michezo. Aliwahi kuwa chini ya kocha Thomas Tuchel aliyetimuliwa msimu ukiopita katika klabu ya Borrusia Dortmund wakati huo wakiwa katika klabu ya Augsburg.

Katika kuthibitisha umri sio kigezo cha kumfanya mtu kukabidhiwa majukumu makubwa hali hiyo inaenda kwa makocha wengine wengi.Makocha kama Diego Martinez Penas anaingia katika mapito haya. Akiwa na umri wa miaka 36 tangu alipozaliwa desemba 16,1980 katika mji wa Vigo pale Hispania.

Diego kwa sasa ndio kocha mkuu wa Osasuna wanaoshiriki ligi daraja la kwanza maarufu kama Segunda.Licha ya kucheza katika klabu ya nyumbani kwao Celta de Vigo na baadae Cadiz alimua kujikita katika ualimu wa soka ili kujipambanua katika upande mwingine wa Michezo.

Katika orodha hiyo unawakuta pia Luis Fransisco Zubeidia kocha wa Derpotivo Alaves akiwa na umri wa miaka 36.

Vijana wengi baada ya kuona njia zilizotengenezwa na watangulizi wao kama AVB na Jose Mourinho wanafikia hatua ya kugundua haina maana ucheze soka daraja la kuu ndipo ufanikiwe kufundisha vizuri.

Wako makocha waliocheza ligi za wilaya huko ulaya na kufikia hatua ya kufundisha soka katika klabu kubwa. Klabu ya Schalke 04 ni moja ya klabu kubwa pale bundesliga. Lakini kocha wao alicheza kwa kiwango cha ligi ya wilaya inayoitwa Kreisliga. Ni ligi ya daraja la chini kabisa lakini haikumfanya kujiona ataishia hapo katika majukumu yake ya ukocha. Akiwa na msomi wa Masuala ya Biashara za uhandisi 'Business engineering' na Msimamizi wa Uvumbuzi 'Innovation management'. Ni Domenico Tadesco Mzaliwa wa Rosaano pale Italia akiwa na miaka 32 sasa. 

Makocha wengi wanofanya vyema hawakucheza kwa kiwango kikubwa nyakati za maisha yao ya soka. Ni wachache ambao weweza kulinda hali ya kipaji cha kucheza na kufundisha soka.

Moja ya usajili wa kwanza kuufanya kocha mkongwe uingereza Harry Rednapp alipowasili katika klabu ya Portsmouth ilikuwa ni Edward John Frank Howe maarufu kama Eddie Howe. Alimsajiki akitokea AFC Bournemouth na hakucheza sana kwani mapema mwanzoni mwa ligi aliumia goti na akaamua kubadili gia kutoka kucheza na kuwa kocha. Alicheza sana AFC Bournemouth na akaanza ukocha hapo kwa kuwa msaidizi wa yimu ya vijana tangu 2008 hadi hivi sasa akiwa na klabu hiyo kama kocha mkuu.

Maisha ya ufundishaji wa soka yako tofauti na Yale uchezaji ndio maana imekuwa rahisi kuona makocha wa wachezaji bora hawakuwahi kuwa na ubora kama huo wa wachezaji wao wanao wafundisha.


Upenyo huu wa vijana katika ukocha unafungua fikra za vijana wengi na kuwafanya wawe wenye ari ya kutaka lujifunza zaidi ili kuja kuwa makocha wazuri.

Ni jambo ambalo halijafanyika kwa soka la Tanzania kwa kupatikana kocha wa chini ya umri wa miaka 35. Na pia dhana ya kufikiria makocha wazuri ni wale waliocheza soka itatoweka taratibu na kuwafanya wale wenye umahili kupata timu za kufundisha. 

Kama ilivyo kwa waamuzi ambako Leo hii tunaona vijana wenye umri wa chini ya miaka 35 wanavyoshika kipyenga ndivyo itakavyokuwa kwa makocha wakuu wa vilabu.
Tunapaswa kutambua karama ya kufundisha ni kitu tofauti na kucheza mchezo wenyewe.


©Nishani Media .co.Ltd
Honorius Mpangala

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad