HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 27, 2017

MAKALA MICHEZO: RATIBA YA VPL INAVYOWANYIMA UTAMU WATEJA WA AZAM TV.


                                                 Na. Honorius Mpangala.

Moja ya kazi ambayo televisheni inayofanikiwa kupata haki ya kurusha matangazo ya soka ni kuweka dau nono na kuratibu vyema vipindi vyake. Uratibu wa vipindi unamhusu sana mtu wa idara ya vipindi kwani anajua namna atakavyoweza kupangilia vyema vipindi ili televisheni iweze kurusha vipindi vyake vyema kama ilivyopangiliwa.

Kushinda tenda ya kurusha matangazo kama ilivyo soka inahitaji upangiliaji mzuri wa ratiba ya Michezo kwa siku husika kama tarehe inavyotaja mchezo utakao chezwa. Televisheni yoyote inayotambua mahitaji ya watazamaji wake kama ilivyo televisheni za mataifa yaliyoendelea yanafanya makubaliano na shirikisho pamoja na bodi ya usimamizi wa ligi ili kuweka muda mzuri wa mechi na kutoa fursa kwa wateja wa kampuni husika inayorusha matangazo kujipatia uhondo unaoendana na kile kilichowafanya wamiliki kisembuzi cha kampuni husika.

Mara nyingi tumeona katika ligi mbalimbali kama ilivyo Hispania, Uingereza au Ujerumani. Mgawanyo wa muda katika kurusha mechi umekuwa mzuri sana na kufanya wapenzi wa soka kutazama Michezo mingi kwa msimu mmoja. 

Upangwaji wa ratiba na muda wa mchezo katika ligi husika unahusisha pande tatu,ikiwepo shirikisho la mpira,bodi inayosimamia ligi pamoja na kampuni yenye haki ya kirusha matangazo ya ligi. Shirikisho hutoa ratiba ya Michezo ya FIFA hiyo inawafanya bodi kutoa ratiba nzuri huku kampuni ya kurusha matangazo ikiweka sawa suala la muda katika kuratibu vipindi vyake siku husika ambapo mechi itachezwa.

Imekuwa kitu cha kawaida kutazama mechi saa nane mchana kwa Masaa ya Tanzania huku Uingereza ikiwa ni saa sita mchana. Vile vile kwa Hispania imekuwa kawaida timu kuingia katika mchezo saa saba mchana hata Ujerumani pia. Hali hiyo hutokana na mpangilio wa vipindi kwa siku husika na hutoa mwanya kwa televisheni kuweza kurusha mechi zaidi ya mbili kwa siku moja kituo kimoja.

Ligi kuu Tanzania ambayo televisheni ya Azam ndiyo wenye haki kurusha mechi zake. Wakati kituo hicho kinapata haki hiyo wengi matarajio yalikuwa ni kutibu kiu ya watazamaji wengi wanaopenda soka la nyumbani. Wakiwa katika morali hiyo inafika wakati kiu yao inashindwa kutibikiwa kutokana na ufinyu wa ratiba katika kurusha mechi kwa utofuati wa muda.

Miundombinu ya Tanzania ni moja ya changamoto nyingine inayofanya tusishuhudie Michezo mingi kwa siku moja. Bodi ya ligi ingeweza kupanga mechi kuanzia saa nane kwa kutazama miundombinu ya uwanja husika na ratiba ya siku ikaishia kwa mechi ya saa mbili usiku

Upangaji huo ungewafanya Azam TV kuweza kukidhi mahitaji ya watazamaji na kujiongezea wigo wa kufanya biashara kwa matangazo.Lazima watoe ushawishi kwa shirikisho na bodi na kufanya wapangile vipindi vyema na kutoa nafasi kwa watazamaji.Nafasi waipatayo watazamaji inaifanya kampuni kuzidi kujipanua kibishara kwani mahitaji ya kisembuzi chao yanaweza kuwa zaidi kutokana na kurusha soka la nyumbani. Soka la nyumbani limewafanya wapenzi wengi wasahau kuhusu matangazo ya redio yanayohusu mpira. Shauku imekuwa kubwa kwao kutaka kuona zaidi na kuwafahamu wanaocheza kuliko kusikiliza.

Ziko mechi ambazo zinakuwa na msisimko nje ya hizi timu hasimu katika ligi yetu. Inapotokea klabu ya Mbeya city wakacheza na Prisons ingefaa Mchezo wao upishane siku hata Masaa na mechi zinazohusu klabu kubwa hapa nchini.Inapotokea Mwadui anacheza na Stand Utd mji wa Shinyanga unakuwa na hamu ya kutazama mechi hiyo kitu ambacho haiwezi kuwapa fursa kutazama kupitia luninga mechi ya Mbeya city na Prisons.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad