HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 27 September 2017

M-KOPA YAIPIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI SANDULA ,MBOZI MKOANI SONGWE

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Wanafunzi wa  shule ya Sekondali Sandula iliyopo wilayani Mbozi imeepukana na changamoto za ukosefu wa umeme pindi wanapojisomea  nyakati za usiku kwa kupatiwa msaada wa vifaa vya umeme wa Jua 'Solar'  kutoka kampuni ya  M-Kopa ikiwa ni mara ya pili kutoa msaada huo katika shule ya sekondari hiyo.

Msaada huo umefanyika  katika Shule ya Sekondari Sandula Wilayani Mbozi  kwa mara ya pili  na shule zingine zilizonufaika na msaada huo ni  shule ya sekondari Mwinyi iliyopo Mkuranga mkoani Pwani  ikiwa ni  kwa ajili kuongeza ufaulu katika shule hizo  kwa kujisomea zaidi katika nyakati za usiku na kuondokana na matumizi ya vibatari vya mafuta ya Taa. 


Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa vya Umeme wa Jua , Meneja Mauzo  M-kopa  Richard  Machera amesema kuwa  kwa Shule ya Sandula uligharimu zaidi ya sh. milioni 4.9 kwa kununua taa za LED sola 36, Chajazasimu, Betri za kuhifadhi nguvu ya Jua  Tisa (9), Paneli Tisa (9), Tochi  Tisa (9) na redio za kisasa za sola Tisa (9)

Vifaa hivyo vimefungwa kwenye madarasa mawili, Ofisi ya Mwalimu Mkuu na Mwalimu Mkuu Msaidizi  pamoja na Mabweni.

Mwalimu Mkuu washule ya sekondari Sandula, Witson Mtafya amesema msaada huo utasaidia  wanafunzi  kupata muda wa ziada wa kujisomea na kufanya mijadala kwenye vikundi kwa fasihi zaidi na hatimaye ufaulu wao utaongezeka.  
 Meneja Mauzo  M-kopa, Richard Machera   akikabidhi Msaada huo vifaa vya umeme wa jua  kwa  Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Sandula Witson Mtafya katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi  mkoani Songwe.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sandula wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi .
 Walimu wa shule wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mauzo  M-Kopa,  Richard   pamoja na wageni waalikwa wengine katika picha ya pamoja. pamoja wakiwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Sandula iliyopo Wilayani Mbozi .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad