HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 21, 2017

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WA JUMUIYA YA MADOLA.

Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Benki ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Benki ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi Fednand Katipwa.
Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Benki ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi Fednand Katipwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili, Ignas Hatusi.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii. 

 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
KWA MARA ya kwanza, nchi ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa jumuiya ya madola utakaofanyika kuanzia Septemba 24 hadi 28 mwaka huu (2017)jijini Dar es Salaam ambapo washiriki kutoka nchi mbali mbali wapatao 354 wanatarijiwa kukuwepo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mahakama ya rufaa, leo jijini Dar es Salaam Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amesema, mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa benki kuu jijini hapa utafunguliwa Septemba 24 na Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Samiah Suluhu Hassan na kufungwa na Rais wa Zanzibar Dkt, Mohamed Ali Shein siku ya Alhamis Septemba 28.

Amesema, mkutano huo wenye maudhui “Mahakama Madhubuti, inayowajibika na Jumuishi” yanayoendana na misingi ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mahakama na nguzo zake tatu utakuwa wa kihistoria kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 1970, kwa mara ya kwanza Tanzania inakuwa mwenyeji.

Amesema, majaji wakuu 13 kutoka nchi mbali mbali na watu mashuhuri wapatao sita ambao ni marais na majaji waandamizi wa mahakama za juu na rufaa kutka Australia, Afrika Mashariki, Pakistani na Zambia wanatarajiwa kushiriki pia huku Mahakama ya Tanzania ikiwakilishwa na wajumbe 50 ambao watakuwa ni majaji na mawakili kutoka Tanzania bara na visiwani.

Ameongeza kuwa, lengo kubwa la mkutano huo ni pamoja na kuwajengea uelewa wajumbe kuhusiana na masuala ya uhuru wa mahakama, mikataba ya kimataifa maendeleo ya kisheria upatikanani wa huduma ya haki, maendeleo ya chama na chagamoto zake katika usikilizaji wa mashauri ambapo pia “Mahakimu na majaji wetu watapata fursa ya kujengewa uwezo na kupata uzoefu juu ya sheria mbali mbali.

Amesema, katika mkutano huo, Tanzania itapata fursa ya kujitangaza kiutalii na vivutio vyake na vile vile itakuza biashara kwa kuongeza kipatao hasa katika mahoteli ambapo wajumbe wengi watafikia.
“Katika kuhakikisha utalii wetu unajitangaza, tumefanya maandalizi ya kutosha na wizara ya mambo ya nadani, wizara ya mambo ya nje na ile ya utalii zinashiriki vema, kwani tunaimani baada ya mkutano huu wageni wengi watabaia nchini na kutembelea vivutio vya utalii na sehemu mbali mbali kama Zanzibar na Bagamyo”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad