HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 4 September 2017

KOREA KASKAZINI YATENGENEZA BOMU LA HAIDROGENI

Korea kaskazini imesema imetengeneza bomu la haidrojeni lenye "uwezo mkubwa wa maangamizi" wakati rais Trump na waziri mkuu wa Japan Abe wamezungumza kwa simu juu ya ongezeka la mzozo wa nyuklia.

Ripoti hiyo iliyotolewa na shirika rasmi la bahari la Korea kaskazini KCNA inakuja wakati kuna hali ya juu ya wasi wasi katika eneo hilo kufuatia majaribio mawili ya makombora yanayoweza kuvuka bara moja hadi jingine mwezi Julai ambayo yana uwezo wa kuruka kiasi ya kilometa 10,000 , na kuyaweka maeneo mengi ya Marekani kuweza kufikika.

Chini ya kiongozi wa kizazi cha tatu Kim Jong Un , Korea kaskazini imekuwa ikiwania kutafuta silaha za kinyuklia ndogo na nyepesi kuweza kuwekwa katika kombora la masafa marefu, bila kuathiri uwezo wake wa kuruka na kulifanya kuwa na uwezo wa kuhimili kuingia katika anga la dunia.

Korea kaskazini , ambayo inafanya mipango yake ya makombora na nyuklia kwa kukaidi maazimio na vikwazo vya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , "hivi karibuni ilifanikiwa" kuitengeneza bomu la hali ya juu kabisa la haidrojeni ambalo linaweza kuwekwa katika kombora la masafa marefu la ICBM, limesema shirika hilo la habari la KCNA.

Bomu hilo la haidrojeni , uwezo wake wa kuripuka ambao unaweza kurekebishwa kutoka mamia ya kilotani na kuwa maelfu ya kilotani, ni bomu la nyuklia lenye uwezo wa aina mbali mbali na uwezo mkubwa wa maangamizi ambalo linaweza kuripuriwa hata katika kima kirefu kwa kutumia vifaa vyenye nguvu kubwa ya shambulizi vya EMP , (electromagnetic pulse) kwa mujibu wa lengo lake la kimkakati, shirika la habari la KCNA limesema.

Hata hivyo Korea kaskazini haijatoa ushahidi wa madai yake ya hivi karibuni, na Kim Dong-yub , mtaalamu wa kijeshi katika chuo kikuu cha Kyungnam wa mitaala ya mashariki ya mbali mjini Seoul, ameonesha shaka.

"Akizungumzia kuhusu mamia kwa maelfu ya kilotani , haionekani kuzungumzia kuhusu bomu hilo la haidrojeni. Inawezekani ni chombo kilichoboreshwa, amesema Kim, alizungumzia kuhusu bomu la atomic ambalo linatumia gesi ya haidrojeni kuimarisha mripuko.

Bomu la haidrojeni linaweza uwezo wa kuripuka wa maelfu ya kilotani , ikiwa na nguvu zaidi kuliko kilotani 10 hadi 15 ambazo jaribio la mwisho la kinyuklia la Korea kaskazini ilifanya mwezi Septemba ambalo ilikadiriwa kutengeneza, sawa na bomu lililodondoshwa mjini Hiroshima , Japan mwaka 1945 na Marekani.

Kim Jong Un, ambaye ametembelea taasisi ya nchi hiyo ya kinyuklia, "aliangalia bomu la haidrojeni litakalowekwa katika kombora linalokwenda masafa marefu na "kuweka mkakati wa kukamilishwa kwa utafiti kuhusu nyuklia," shirika la habari la KCNA limesema.

Picha zilizotolewa na shirika hilo la habari zinamuonesha Kim akikagua silaha yenye rangu ya fedha katika ziara hiyo akifuatana na wanasayansi wa nyuklia , wakiwa na mchoro wa kombora la Hwasong-14 likionekana ukutani.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre
Mhariri: Sudi Mnette

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad