HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 14 September 2017

JUMIA waja na mfumo wa malipo ya kulipa baada ya kupokea bidhaa


 Maneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi Kampuni ya Jumia Tanzania inavyoweza kurudisha imani kwa watanzania namna ya kununua bidhaa mtandaoni kwa kutumia mfumo wa malipo baada ya mteja kupokea bidhaa yake kwenye ofisi zao Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mkuu wa Biashara wa Jumia Tanzania, Mikolaj Kucia akizungumza na waandishi wa habari namna ya malipo yanavyofanyika hasa pale tu mtu anapopokea bidhaa wanzaouza mtandaoni pamoja na namna wanavyofikisha bidhaa kwa wateja wao kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi zao Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo.
Kampuni inayojihusisha na huduma za manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia ya mtandao nchini, Jumia Tanzania imewaondolea hofu wateja wake kwamba sasa wanaweza kulipia bidhaa pale zinapowafikia baada ya kufanya manunuzi kupitia tovuti yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Bw. Albany James amebainisha kwamba wameona ni vema kuutambulisha mfumo huo mpya kwa wateja wao ili kuwaondolea hofu na kuwajengea uaminifu kwa huduma zote za manunuzi wanazozifanya kwa njia ya mtandao.
Jumia Tanzania inayo furaha kuwajulisha wateja wao wote kwamba hivi sasa wanaweza kulipia bidhaa wanazozinunua kwa njia ya mtandao pindi zinapowafikia. Tumeona ni vema kuwapa wateja wetu chaguo hilo kwa kuzingatia mila na tamaduni tulizonazo watanzania kwamba tumezoea kununua bidhaa baada ya kujiridhisha kwa kuiona kwa macho. Mbali na hapo bado teknolojia ya huduma na manunuzi kwa njia ya mtandao ni ngeni miongoni mwa watanzania wengi hivyo wanakuwa na hofu kwamba wanaweza kuwa wanatapeliwa,” alisema Bw. James.
“Faida nyingine mbali na mteja kuiona bidhaa aliyoiagiza na kujiridhisha ndiyo alipie pia mteja atapata fursa ya kuweza kubadilisha kama hatoridhika. Tumekuwa tukipokea changamoto kwa baadhi ya wateja wetu kwamba wamekuwa wakipelekewa bidhaa ambazo zimekuwa tofauti kidogo na walivyoagiza. Ingawa tunawasisitiza sana kuwa makini na kuzingatia taarifa muhimu za bidhaa wananozitaka lakini katika kuwathibitishia kwamba Jumia Market sio wababaishaji tumeamua kuwajulisha kwamba wana chaguo la aidha kulipia kwa njia ya mtandao au pale bidhaa inapomfikia,” aliongezea Meneja Masoko huyo wa Jumia Tanzania.
Aliendelea mbele kwa kuongeza zaidi kwamba tofauti ya Jumia Tanzania na kampuni zingine zinazojihusisha na huduma za mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao ni kwamba wao pekee ndio wanawapa wateja wao chaguo la kulipia bidhaa pale zinapowafikia. Na pale mteja asiporidhika na bidhaa aliyopelekewa anao uwezo wa kuomba kubadilishiwa na kuletewa bila ya kudaiwa malipo yoyote.
“Ningependa kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia ofa mbalimbali za manunuzi ya bidhaa kwenye tovuti yetu na mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Instagram. Lakini pia kwa wafanyabiashara wa kitanzania kuhamia kwenye njia za mitandao ili kupanua wigo wa wateja wao. Kuna faida nyingi za kujiunga nasi zikiwemo kujiongezea wateja wengi tofauti na wale wanaotembelea maduka yao moja kwa moja lakini pia kutangazwa bure kabisa bila ya malipo yoyote kwenye mtandao wetu,” alihitimisha Bw. James.
Jumia Tanzania ina amini kuwa tekinolojia inavyokua kwa kasi inatubidi kwenda nayo sambamba hasa kwenye manunuzi ya bidhaa tajwa hapo juu ili kuepuka usumbufu wa kuzunguka duka hadi duka pamoja na kuokoa muda kwasababu bidhaa zote zinazoagizwa hupelekwa hadi pale mteja alipo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad