HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 19, 2017

JOTUN yafungua Duka lake la Rangi jijini Dar

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru (watatu kutoka kulia) akikata utepe katika ufunguzi wa Duka la vifaa vya Ujenzi la Jotun Tanzania, lililopo Mtaa wa Mkwepu, Posta Mpya jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Norway nchini, Bi. Hanne Marie Kaarstad na wa pili kushoto ni Makamu Rais wa JOTUN, Esben Hersve. Kampuni ya Jotun iliyoanzishwa nchini Norway mwaka 1926, ni moja ya kampuni zinazoongoza katika uzalishaji wa rangi duniani, ambapo mwaka 1974 Jotun waliweka uwepo wao katika nchi za umoja wa nchi za kiarabu, tangu wakati huo Jotun imekuwa ikikuwa katika maeneo tofauti, na kuwa kampuni pekee ya uzalishaji rangi  iliyopata tunzo ya vyeti vya viwango vya ubora vyenye  namba  ISO 9001: 2008, ISO 14001 & OHSAS 18001. Kampuni hii pia ina viwanda vya uzalishaji katika nchi ya Abu Dhabi, Dubai, Saudi Arabia, Oman na Misri.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru, akipewa maelekezo ya namna mashine ya uchanganyaji rangi inavyofanya kazi toufauti kwa dakika moja.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru, akihutubia katika sherehe za ufunguzi wa duka la rangi ya Jotun Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad