HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 11 September 2017

JESHI LA POLISI MKOANI KUSINI PEMBA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

Jeshi la polisi mkoa Kusini Pemba linamshikilia mwanamke moja kwa tuhuma za  kukamatwa  akiwa na furushi linalotiliwa mashaka kuwa ni  madawa ya kulevya lenye kete 3621 unao kisiwa kuwana thamani ya zaidi ya sh milioni 7  akitokea Bandarini mkoani  kueleka Jadida Wete.

Kwamujibu wa taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Kusini Pemba kamishina msaidizi mwandamizi Mohamed Shekhani Mohamed  amesema mwanamke huyo aliyekuwa amevaa shungi jeusi la stara ya mwanamke  na kisha kulificha furushi hilo  ndani ya shungi la baibui alilovaa  walifanikiwa kumkamata baada ya kuulizwa hali na askari alie kuwepo barabarani na kuanza kujenga hofu iliyompa mashaka askari huyo ndipo walipo mueka chini ya ulinzi na hatua zakisheria ilikuweza kumpekuwa zikafata na kupatikana na kete hizi 3621 zilizotiliwa mashaka kuwa za madawa ya kulevya.

Amesema idadi hiyo waliyoikamata ni kubwa ukilinganisha na kesi takriba 21 za madawa ya kulevya  ambazo wamekwisha kuzikamata tokea kuanza kwa msako dhidi ya madawa ya kulevya mkoani hapo. 

Kamanda amewataka wananchi kuacha tabia ya kuyatumia mavazi ya heshima kama chaka la kusafirishia madawa ya kulevya na kwamba mbinu hiyo tayari  polisi  mkoa Kusini Pemba wamekwisha igundua.

Kamanda amesema  zaidi ya kesi 21 zimekamatwa tokea kuanza masako huo wa madawa ya kulevya polisi Kusini Pemba saba wamekwisha fungwa 11 zipo mahakamani huku nne zikitarajiwa kutolewa hukumu wakati wowote .

Chanzo: ITV Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad