HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 18, 2017

DAWASCO YALALAMIKIWA KWA KWAKERO MAJI YANAYOTAPAKAA KATIKA MTAA HUO.

WAKAZI  wa Mtaa wa Sinza uliopo katika Mhakama ya Mazese walalamikia  kero wanayoipata kutokana na miundombinu mibovu ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) yanayosababisha maji kutapakaa barabarani hususani katika mtaa huo ambao ndani yake ipo Mahakama ya Mazese Mpaka njiapanda ya kuelekea Ukumbi wa Mirado jijini Dar es Salaam.

Malalamiko hayo yametolewa na Wakazi wa Maeneo hayo ambao hawakutaka kujulikana wakati Akizungumza na mwandishi wa Michuzi Blog jijini Dar es Saalam leo. 

Pia amewaomba watendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Maji  taka(DAWASCO) watembelee katika eneo hilo ili waweze kufanya marekebisho ya bomba hilo kwani maji mengi sana yanapotea katika eneo hilo ambapo yakikanyagwa na magari yanakuwa machafu sana yanayoleta kinyaa pamoja na usumbufu kwa wapita njia.

"Tunawaomba watendaji wa DAWASCO watembelee eno hiyo ili waweze kufanya marekebisho ya bomba linalotiririsha maji mengi sana yanayofika mpaka barabara ya Shekilango-Sinza."

Pia amesema kuwa  "nikiasi gani cha maji yanayopotea katika eneo hilo kwani yanaharibu hata barabara za mitaa mtaa wetu kama vile kunamvua  hadi tunaonekana wakazi wa mtaa huu waa Sinza ni wachafu kupindukia"

Pia amewaasa wafanyakazi wa DAWASCO watembelee maeneo mbalimbali ili kujionea upotevu wa maji ambayo ni mhimu kwa matumizi ya binadamu pamoja na wanyama.
 Mwonekano wa maji yanayotiririka katika mtaa wa Sinza.
 Mtaa wa sinza ukiwa ma maji kila kona ikiwa yanasababisha usumbufu mkubwa kwa wapitanjia.

 Mwonekano wa Mtaa wa Sinza.
 Maeno hayo yamelowa maji ya DAWASCO.

 Mwonekano wa barabara inayotokea Ukumbi wa Mirado jinsi ulivyolowa maji ya wahusika.
 Maji yaliyotuwama kandokando ya ukuta wa Mahakama ya Mazese jijin Dar es Salaam.
 Mwonekano wa Maji ambayo yamefanya Matope Mbele ya Geti la Mahakama ya Mazese liyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Maji yametuama karibu kabisa na Geti la mkazi wa maeneo hayo yanayosababisha mkazi huyo kutoweza kutokea geti hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad