HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 13 September 2017

BOSI WA ZAMANI WA ATCL, DAVID MATAKA NA MWENZAKE WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MIL 70 AU KIFUNGO CHA MIAKA SITA JELA

 Na Karama Kenyunko,blogu ya Jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka (66) na  Kaimu Ofisa Mkuu, Kitengo cha Fedha, Elisaph Mathew, kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 70, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa washtakiwa walitenda makosa.

Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwemo kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara kwa  shirika hilo. Mahakama hiyo pia imewataka washtakiwa hao kugawana hasara waliyoisababisha ambayo ni dola za Marekani 143,442.75 na kuilipa kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imemuachia huru aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William Haji ambaye alikuwa mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake bila ya kuacha shaka.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa ambaye akisoma hukumu hiyo alisema mahakama imezingatia kigezo cha washitakiwa kuwa wakosaji wa kwanza na kwamba taratibu za utoaji wa adhabu zimeelekezwa na mahakama kuu ya kulipa faini au kifungo.

Amesema kuwa upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka kwa kuleta mashahidi 14 kwa ajili ambao ushahidi wao umeweza kuwatia hatiani Mataka na Elisaph.

Amesema, katika shitaka la kwanza washitakiwa kila mmoja anatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kwenda jela miaka mitatu huku katika mashitaka ya kutumia madaraka vibaya, pia wanatakiwa kulipa faini ya milioni tano kila mmoja au jela miaka mitatu wakati kosa la sita la kuisababishia ATCL hasara walipe Sh milioni 10 au kifungo cha miaka sita.

Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliomba mahakama itoe adhabu kali kwa kwa washtakiwa na kwamba hawana rekodi ya makosa ya nyuma ya washitakiwa hao.

Katika utetezi wake Mattaka alidai anaishukuru mahakama kwa kuona wema wao wa kuiokoa ATCL mpaka walipofikia na kwamba taarifa walizonazo magari waliyonunua ndio yanayotumika hadi sasa kwani hawajaingiza mengine.

Aidha amesema yeye ni MTU mzima,  anamiaka 66, anasumbuliwa na shinikizo la damu, familia inayomtegemea Poa mama take mzazi no mzee Wa miaka 85 na yeye ndiye anamtunza.

Kwa upande wake Mathew amesema yeye ni Askofu wa Kanisa la motomoto Pentekoste na kuiomba mahakama kuwa anataka kuhubiri injili ya Yesu Kristo na kwamba anaomba adhabu atakayopewa imiwezeshe kuendelea na uhubiri pia anaomba msamaha kwani anafamilia inayomtegemea.

Wakili wa utetezi, Francis Mgale alidai ni mara ya kwanza kwa mshitakiwa Mathew kufanya kosa hivyo mahakama impunguzie adhabu na iangalie mazingira yaliyowakuta ATCL hadi kutiwa hatiani.

Mattaka na mwenzake walishitakiwa kwa mashitaka sita ikiwemo ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya dola 143,442.75 za Marekani.

Kati ya Machi na Julai 2007, wakiwa watumishi wa umma, walikula njama ya kutenda na kutumia madaraka yao vibaya kwa kuidhinisha ununuzi wa magari yaliyotumika 26 kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Pia inadaiwa kati ya Juni na Julai 2007 wakiwa maofisa wa ATCL katika kutekeleza majukumu yao walikaribisha zabuni ya ununuzi wa magari 26 bila kufuata taratibu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad