Na Agness Francis , Globu ya Jamii.
Mtandao wa wasanii wote wa tasnia ya injili na maadili ya Utaifa, Tanzania Gospel Artists Nertwork (TAGOANE) wamekabidhiwa cheti kilicho sajiriwa kisheria kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia chombo chenye dhamana BASATA na kupewa namba ya usajiri BST/00020 kwa mujibu wa sheria Na.23 ya mwaka 1984.
Zoezi hilo limeongozwa na Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza ambaye ndiye amekabidhi cheti hicho leo katika ofisi zake zilizoko BASATA Ilala Sharif Shamba Jijijni Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza amesema kuwa maadili mema huleta amani kwa wananchi na amewapongeza wasanii hao kwa hatua waaliofikia hadi sasa kwa kutembelea mikoa tofauti tofauti nchini kwa lengo la kuwaunganisha na fursa mbalimbali ulimwenguni katika kukuza huduma na kukua kiuchumi .
Hata hivyo Rais wa TAGOANE , Godwine Maimu Nnyaka ametanabaisha kuwa watashirikiana na Seriakali katika kukuza pato la taifa kwa kudhibiti wauzaji haramu, wanyonyaji na matapeli wa kazi za wasanii kwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa dhumuni la kuongezea kipato Taifa na kwa wasanii pia.
Nae Katibu mkuu TAGOANE, Mchungaji Lucy Wilson ametoa wito kwa wakidada na wakinakaka wajitokeze kwa wingi kujiunga na mtandao huo wa wasanii wote wa tasnia ya injili na maadili ya utaifa na waichukulie sanaa ya injili kama kazi zingine.
Rais wa TAGOANE , Godwine Maimu Nnyaka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwaunganisha wasanii wote wa Tasnia ya Injili ili kuwa na sauti moja na lugha moja ili kufikia malengo yao kiroho na kimwili leo walipokuwa wakikabidhiwa cheti na BASATA cha kutambua umuhimu wa wasanii wa sanaa ya tasnia ya Injili.
Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza akimkabidhi cheti cha kutambua umuhimu wa wasanii wa sanaa ya tasnia ya Injili kwa Rais wa TAGOANE , Godwine Maimu Nnyaka leo jkatika ofisi za BASATA jijini Dar.
Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza akiwapongeza Viongozi wa wasanii wote wa Tasnia ya Injili kwa hatua waliofikia kwa kutembelea baadhi ya mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwaunganisha na fursa mbalimbali ulimwenguni katika kukuza huduma na kukua kiuchumi
Baadhi ya viongozi wa wasanii wote wa Tasnia ya Injili pamoja na wasaii wakiwa kwenye picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment